Ni kwamba utafika mahali na wewe uanze kujidanganya mwenyewe.
Ukishawadanganya sana watu, wakaamini kile unachowadanganya, utaanza kushawishika kwamba huenda unachodanganya ni ukweli na unaanza kuamini uongo wako mwenyewe.
Japo ndani yako kabisa utaendelea kujua ni uongo, lakini utayajenga maisha yako kwenye uongo huo na matokeo yake hayatakuwa mazuri.
Tatizo jingine la kudanganya ni kwamba unahitaji uongo mkubwa zaidi kufunika uongo wa mwanzo. Hivyo uongo mmoja unazaa uongo mwingine, ambao nao unazaa uongo mwingine, mpaka unakuja kujikuta kwenye hatua ambayo hukutegemea ungefika.
Uongo uliokuwa umeanza kidogo unakuwa mkubwa kiasi cha wewe mwenyewe kushindwa kujua utaishia wapi.
Maisha pekee ya uhuru ni kuwa mkweli, sema ukweli kama ulivyo, hata kama unakuumiza wewe au kuwaumiza wengine. Ukweli unahitaji kusemwa mara moja tu, na baada ya hapo kila mtu anaendelea na maisha yake.
Lakini uongo unahitaji kusemwa tena na tena na tena na lazima uishi kwa maigizo ili uongo huo usigundulike kwamba ni uongo.
Mara zote sema ukweli, utaondokana na matatizo mengi sana.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,