Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari NGUVU HAIPOTEI…
Ipo kanuni ya kisayansi inayosema kwamba nguvu haiwezi kutengenezwa wala kupotezwa, bali inaweza kubadilishwa kutoka kwenye mfumo mmoja kwenda mwingine.
Mfano mkaa una nguvu ya kikemikali, ukiuchoma nguvu hiyo inabadilika kwenda nguvu ya mwanga na joto.

Kadhalika kwenye maisha yetu, nguvu tayari tunayo.
Nguvu ya kufanikiwa au kushindwa tayari ipo ndani yetu.
Hatuwezi kitengeneza wala kupoteza nguvu hii.
Badala yake tunaweza kuihamisha kutoka eneo moja kwenda eneo jingine.

Ili kufanikiwa, unahitaji kutumia nguvu ile ile ambayo unaitumia kabla hujafanikiwa.
Nguvu ile ile unayoitumia kutoa sababu sasa, nguvu ile ile unayoitumia kwenye mambo yasiyo muhimu, nguvu ile ile unayoitumia kufuatilia maisha ya wengine, ndiyo nguvu utakayoweza kuitumia kutengeneza mafanikio makubwa kwako.

Usijiulize unapata wapi nguvu, bali jiulize unahamisha nguvu kutoka wapi. Maana nguvu tayari unazo, ila unazitumia kwenye sehemu isiyo sahihi kwako.
Ili uwezw kufanya unachotaka, unahitaji kuacha baadhi ya vitu unavyofanya sasa, maana hivyo ndiyo vinatumia nguvu zako na kukuzuia usitumie nguvu hizo kwenye kile unachotaka.

Anza leo kuelekeza nguvu sahihi kwenye maeneo sahihi ya maisha yako, na utaweza kupiga hatua kubwa sana kufika unakotaka kufika.

Ukawe na siku bora sana yaleo, siku ya kutumia vizuri nguvu zako kwenye yale maeneo ambayo ni muhimu zaidi kwako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha