Normal
0

21

false
false
false

SW
X-NONE
X-NONE

/* Style Definitions */
table.MsoNormalTable
{mso-style-name:”Table Normal”;
mso-tstyle-rowband-size:0;
mso-tstyle-colband-size:0;
mso-style-noshow:yes;
mso-style-priority:99;
mso-style-parent:””;
mso-padding-alt:0in 5.4pt 0in 5.4pt;
mso-para-margin-top:0in;
mso-para-margin-right:0in;
mso-para-margin-bottom:8.0pt;
mso-para-margin-left:0in;
line-height:107%;
mso-pagination:widow-orphan;
font-size:11.0pt;
font-family:”Calibri”,sans-serif;
mso-ascii-font-family:Calibri;
mso-ascii-theme-font:minor-latin;
mso-hansi-font-family:Calibri;
mso-hansi-theme-font:minor-latin;
mso-bidi-font-family:”Times New Roman”;
mso-bidi-theme-font:minor-bidi;
mso-fareast-language:EN-US;}

Wapo watu ambao huwa wanasumbuliwa sana na shambulio la mshtuko, kitu fulani kinatokea na kuwashtua sana kiasi kwamba wanaogopa au kuhofia kabisa kufanya kitu hicho au hata kingine.

Mara nyingi watu huwa wanakuwa na mipango mizuri wanapoanza kitu chochote, lakini wanapoendelea kufanya, wanakutana na changamoto, ambayo inavuruga mipango yao, na hapo kila kitu kinaharibika.

Ukweli kuhusu maisha ni kwamba, hakuna kitu kitakachoenda kama unavyopanga au kutaka kiende. Mambo mengi yatakwenda tofauti na ulivyotegemea yaende, mambo mengi yatakwenda kwa mvurugiko mkubwa.

Kitu pekee kitakachokusaidia wakati mambo yanaenda tofauti na ulivyopanga, wakati mambo yamevurugika, ni jinsi utakavyokuwa umetulia.

Nje panapotibuka na kuvurugika, ndani panapaswa kutulia sana. Pale ambapo mipango yote uliyoweka haifanyi kazi, ndani yako unapaswa kuwa na utulivu wa hali ya juu sana.

Hii ndiyo njia pekee itakayokuwezesha kuvuka changamoto unazokutana nazo. Kwa sababu unapokuwa na utulivu ndani yako, unaweza kufanya maamuzi sahihi na kuchukua hatua sahihi.

Lakini pale nje panapovurugika, na ukaruhusu mawazo yako nayo yavurugike, utashindwa kabisa kufanya maamuzi sahihi na kushindwa kuchukua hatua sahihi.

Kazana sana kuwa na utulivu ndani yako bila ya kujali nini kinaendelea nje, hata kama kila mtu yupo kwenye taharuki na kukimbilia kufanya maamuzi ya haraka, wewe kuwa na utulivu na fanya maamuzi sahihi.

Utulivu wako wa ndani ndiyo utakaokuwezesha kushinda kwenye chochote unachofanya. ukikosa utulivu wa ndani, kitu kidogo sana cha nje kitakuzuia kufika unakotaka.

Na hata watu wakijifunza kwamba huna utulivu wa ndani, watakuwa wanakuvuruga makusudi ili wapate kile wanachotaka wao.

Kila la Kheri Rafiki Yangu.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha