Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAISHA NA KIFO…
Ili kuwa na maisha bora,
Ili kuweza kufanya yale ambayo ni muhimu sana kwetu,
Ili kuweza kuwajali wale ambao ni wa muhimu kwa maisha yetu,
Tunahitaji kuwa na mawazo mawili kinzani kila wakati, mawazo ya maisha na kifo.
Unahitaji kufikiri kwamba utaishi miaka 100 zaidi, na wakati huo huo unahitaji kufikiri kwamba leo ndiyo siku yako ya mwisho ya kuishi.
Kwa kuwa na mawazo haya mawili kwa wakati mmoja, inakuwezesha kuchukua hatua ambazo ni sahihi kwako sasa na hata baadaye.
Kabla hujachagua kufanya chochote jiulize maswali haya mawili;
Je kwa kufanya kitu hichi, kitakuwa na manufaa au kikwazo gani kwangu kwa miaka 100 ijayo?
Swali la pili, je kama leo ndiyo siku ya mwisho ya maisha yangu, kuna umuhimu wa kufanya hili?
Kuwa na mawazo haya kuhusu maisha na kifo siyo kwa ajili ya kujipa hofu ai kufikiri hasi.
Bali ni kwa ajili ya kufikiri uhalisia wa maisha.
Kwa sababu unapofikiri utaishi miaka 100 zaidi, utafanya maamuzi ambayo hayatakuwa kikwazo kwako baadaye.
Na unapofikiri kwamba leo ni siku yako ya mwisho kuishi, hutafanya mambo ya kupoteza muda wako, kwa sababu huna muda wa kupoteza.
Na ukiangalia fikra zote ni sahihi, kwa sababu unaweza kuishi zaidi na pia unaweza kufa muda wowote.
Hivyo ni vyema kuweka mkazo kwenye yale ambayo hi muhimu zaidi ili maisha yako yaweze kuwa bora kabisa.
Ukawe na siki bora sana ya leo, siku ya kuishi kama ndiyo mwanzo wa maisha yako, na pia kuishi kama ndiyo mwisho wa maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha