Mpendwa rafiki,

Kila mmoja wetu ni mwekezaji huenda hata wewe ulipo kuna sehemu umewekeza unategemea upate faida baada ya kuwekeza. Tofauti yetu ni aina ya uwekezaji tunaofanya, kuna wengine wanawekeza vitu ambavyo ni hasi havina msaada kwao na kuna kuna wengine wanawekeza vitu chanya vyenye msaada kwao.

Muda mzuri wa kufanya uwekezaji ni sasa, sasa ndiyo muda bora kwako kwa sababu una nguvu lakini watu wengi wanakuja kushtuka na kufanya uwekezaji fulani wakiwa tayari umri umeenda, wanakuja kujilaumu na laiti ningelijua. Kwa mfano, kama mtu ni mara yake ya kwanza kupata maarifa ataanza kujilaumu hivi kwanini sikukujua mapema yaani ningekuwa mbali sana kwa maarifa haya ninayopata. Muda mzuri ni kwako, hivyo jua na wajibika katika kile ulichochagua usipoteze muda katika maneno ambayo hayana msaada katika maisha yako.

Growth

Aliyekuwa mmoja wa mababa, na mwasisi wa taifa la marekani Benjamini Franklin aliwahi kunukulikwa akisema; uwekezaji katika maarifa huwa unalipa kwa riba bora.  Huwa tunakwepa sana uwekezaji wa maarifa lakini baadaye tunakuja kulipa gharama tena kwa riba kubwa sana, hakuna mtu ambaye alishawahi kufilisika kwa sababu eti anawekeza sana katika maarifa, maarifa ni uwekezaji mzuri unaolipa kabla hujaungia katika aina nyingine za uwekezaji basi uwekezaji wa kwanza ambao kila mtu anayetaka kuwa mwekezaji anatakiwa kuufanya ni uwekezaji wa maarifa.

Wengi wanaingia katika kuwekeza eneo fulani wakiwa hawana maarifa wanajikuta wanaanguka vibaya, gharama ambao walikuwa wanaikwepa inakuja kuwa kubwa zaidi ya ile ambayo angetakiwa kulipa. Watu bado hawajaamka katika kulipia maarifa, tumeshazoea watu kufanya shopping za nguo lakini siyo za vitabu. Dunia ya sasa inahitaji uwe mwekezaji mzuri wa maarifa ndiyo utaweza kufurahia na kukabiliana na kila hali kwa sababu bila maarifa ni sawa na kwenda sehemu ambayo huijui.

SOMA;Hii Ndiyo Nyumba Adimu Sana Kupatikana Katika Zama Hizi Za Taarifa.

Ukiambia uchangie gharama katika maarifa unaona ni kama mzigo lakini pale unapoanguka unaanza kuyatafuta maarifa kwanini sasa mpaka uanguke ndiyo utafute maarifa? Jiandae mapema, kila siku hakikisha unakuwa bora, soma vitabu, sikiliza au angalia maarifa chanya yatakayoweza kukusaidia kutoka hatua moja kwenda  nyingine.

Hatua ya kuchukua leo, wekeza katika maarifa kwanza kabla hujaanza kwenda kuwekeza sehemu nyingine. Anza kuwa rafiki wa kulipia maarifa na kuyafurahia na kuyafanyia kazi pale unapoyapata.

Hivyo basi, hakuna ambaye anawekeza katika maarifa halafu huwa anabaki kama alivyo, ukitaka kufanikiwa eneo fulani ulilochagua anza kuwekeza kwanza katika maarifa.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki yangu.

Rafiki na mwalimu wako,

Deogratius Kessy

0717101505/0767101504

deokessy.dk@gmail.com , kessydeo@mtaalamu.net

Unaweza kutembelea tovuti yangu kwa kujifunza zaidi kila siku na kupata huduma mbalimbali kama vile vitabu, kwa kutembelea tovuti  hii  hapa  www.mtaalamu.net/kessydeo .

Asante sana na karibu sana !