Rafiki yangu mpendwa,
Kama ambavyo nimekuwa nakupa taarifa mara kwa mara, semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka huu 2018 itafanyika tarehe 03/11/2018 jijini Dar Es Salaam. Ni semina ya kukutana ana kwa ana ambapo tunakwenda kujifunza mengi sana kuhusu maisha ya mafanikio makubwa.
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA ni tukio la mwaka ambalo mtu yeyote aliye makini na mafanikio yake hapaswi kulikosa. Kwa sababu kwa kushiriki semina hii, unaondoka ukiwa na maarifa na hamasa kubwa ya kwenda kufanyia kazi kwa kipindi cha mwaka mzima.
Leo nakwenda kukushirikisha walengwa wakuu wa semina hii, na hatua za kuchukua ili usikose kushiriki semina hii bora sana kwako kwa mwaka huu 2018.
Miaka ya nyuma, semina za KISIMA CHA MAARIFA, zilikuwa maalumu kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA pekee. Lakini enzi hizo KISIMA CHA MAARIFA hakikuwa kinamhitaji mtu afanye kazi sana ili kuwepo. Ilikuwa unalipa tu ada na kujiunga. Lakini sasa hivi KISIMA CHA MAARIFA kimebadilika, kulipa ada pekee hakukutoshi kuendelea kuwa mwanachama, kuna hatua lazima uchukue ili uendelee kuwa mwanachama. Mfano kuwa na vyanzo mbadala vya kipato, kujifunza kupitia usomaji wa vitabu, na kuyapima maisha yako kila mwezi.

Kwa vigezo hivi vipya vya KISIMA CHA MAARIFA, siyo wengi kitawafaa, maana wengi wanataka tu kujifunza, hawataki kufuatiliwa fuatiliwa sana. Hivyo watu hawa nawapa nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA, hata kama siyo wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.
Hii ni kusema kwamba, mtu yeyote anayependa kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka huu 2018 anaweza kushiriki awe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA au la.
Na pia kwa mtu yeyote aliyepanga kushiriki, unaweza kuja na mtu ambaye unaona anaweza kujifunza zaidi kupitia semina hii. Anaweza kuwa mwenza wako, ambapo mtajifunza kwa pamoja jinsi ya kuendesha maisha yenu. Anaweza kuwa mbia mwenzako kwenye biashara ambapo mtajifunza kwa pamoja jinsi ya kuboresha biashara yenu. Anaweza kuwa msaidizi wako kwenye biashara ambapo atajifunza jinsi ya kuweka juhudi zaidi kwenye biashara yako.
Karibu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018, na njoo na wengine ambao unaona wanaweza kunufaika na semina hii bora sana kwa mwaka huu 2018.
Hivyo nijumuishe kwa kusema, ushiriki wa semina upo wazi kwa watu wote, bila ya kujali ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA au la. Pia ni vyema ukaambatana na mtu mwingine wa karibu kwako au unayeshirikiana naye kwenye yale unayofanya naye akajifunza.
Baada ya kukushirikisha hilo muhimu sana kuhusu semina, sasa nikuambie walengwa wakuu wa semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018.
Wafuatao ndiyo walengwa wakuu wa semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, kama una sifa yoyote kati ya hizi basi chukua hatua sasa kuhakikisha unashiriki semina hii;
- Kama una kiu kubwa ya kupiga hatua kwenye maisha yako, unatamani kwenda mbali zaidi ya hapo ulipo sasa, basi semina hii inakuhusu sana.
- Kama unajua kuna uwezo mkubwa ambao upo ndani yako, lakini bado unaona hujaweza kuutumia vizuri, njoo kwenye semina na utaweza kuona jinsi ya kutumia uwezo huo.
- Kama unapenda kufikia utajiri na uhuru wa kifedha kwenye maisha yako, kama unataka kuacha kuwa na hofu ya fedha kila wakati, usikose semina hii.
- Kama umejaribu vitu vingi kwenye maisha yako lakini vyote umeshindwa, kama unajiona wewe upo kwenye kundi la wale ambao hawawezi kufanikiwa, shiriki semina hii.
- Kama upo kwenye ajira na kipato chako pekee ni mshahara, ambao umekuwa haukutoshi na maisha ni magumu, njoo kwenye semina upate mbinu za kuongeza kipato chako.
- Kama umeanzisha biashara lakini haikui, au umeshaanzisha biashara nyingi na zinakufa, kuna tatizo mahali, ambapo kwa kushiriki semina hii utajua wapi unakosea.
- Kama unataka kuacha alama kwenye hii dunia, kama unataka kuifanya dunia kuwa sehemu bora zaidi ya kuishi, basi shiriki semina hii.
- Kama watu wanaokuzunguka hawakuelewi au wanakudharau, wanakuchukulia kama mtu ambaye hakuna kikubwa unaweza kufanya kwenye maisha yako, kama wanakuambia huwezi na utashindwa, njoo ukutane na washindi wengine watakaokupa hamasa ya kushinda zaidi.
- Kama wewe ndiyo biashara yako, yaani kama biashara unayoendesha inakutegemea wewe kwa kila kitu, ukiondoka basi biashara inasimama au inasua sua, njoo ujifunze jinsi ya kutengeneza mifumo itakayoiwezesha biashara kujiendesha yenyewe hata kama haupo kabisa. Hapa ndipo utakapopata uhuru kamili wa kibiashara.
- Kama unataka kukutana na Kocha Dr Makirita Amani ana kwa ana, na kujifunza kwake, kumuuliza maswali mbalimbali ambayo yamekuwa yanakutatiza, basi nafasi pekee ni hii ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018.
Semina hii itakuwa ni siku moja, masaa 12 ya kujifunza, kuhamasika, kukuza mtandao wako na kuwapata watu sahihi wa kushirikiana nao na hata kujifunza kwao. Kama una sifa yoyote kati ya hizo hapo juu na nyingine zinazoendana na hizo, usikubali kabisa kukosa semina hii. Fanya lolote uwezalo, kuhakikisha unashiriki semina hii muhimu sana kwa mafanikio yako.
JINSI YA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA.
Tarehe ya semina ni 03/11/2018.
Ada ya kushiriki semina hii ni tsh 100,000/= (laki moja) ambayo itajumuisha chai, chakula, vitabu vya kutumia wakati wa semina na huduma nyingine muhimu.
Tarehe ya mwisho kulipa ada ya kushiriki semina hii ni 31/10/2018.
Tarehe ya mwisho kudhibitisha kushiriki semina hii ni 01/10/2018.
Utaratibu wa kulipa ada ni unaweza kulipa kidogo kidogo, kila siku, kila wiki na kila mwisho wa mwezi mpaka kufikia tarehe 31/12/2018.
Jinsi ya kulipa, unatuma ada kwa namba 0717396253 au 0755953887 majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA.
Ukishatuma ada, tuma ujumbe wenye majina yako kamili na kwamba umelipa ada ya kushiriki semina kwenda namba 0717396253.
Kudhibitisha kushiriki semina hii, tuma majina yako kamili, na namba ya simu na ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717396253.
Karibu sana rafiki yangu kwenye semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2018, semina muhimu sana kwako kwa mwaka huu 2018. Dhibitisha sasa kwamba utashiriki semina hii kwa kutuma majina na namba ya simu kwenda namba 0717396253. Pia anza kulipa ada sasa ili mpaka kufika tarehe 31/10/2018 uwe umekamilisha na ujihakikishie kushiriki semina.
Kama umekuwa unasoma makala zangu kwa muda sasa, nina hakika kuna kitu unajifunza, la sivyo usingepoteza muda wako, maana najua una mengi ya kufanya. Hivyo nikukaribishe ujifunze kwa ukaribu zaidi kwenye semina yetu ya mwaka huu 2018, nategemea kukuona pale kwenye semina. Chukua hatua ya kudhibitisha sasa, kama hujafanya hivyo ili ujipatie nafasi yako.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha
Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; http://eepurl.com/dDZHvL