Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NDIYO YAKO NA HAPANA YA WENGINE…
Umekuwa unaipa hapana ya wengine uzito mkubwa kuliko ndiyo yako binafsi.
Umekuwa unathamini zaidi maoni ya wengine kwa nini unaweza na nini huwezi kuliko maoni yako binafsi.
Watu wakikuambia HAPANA unakubaliana nao, hata kama ndani yako kuna NDIYO.
Na hili limekuwa kikwazo kikubwa sana kwenye mafanikio yako.
Ili kufanikiwa, NDIYO yako inapaswa kuwa kubwa kuliko HAPANA ya wengine.
Unahitaji kujiwekea kipaumbele kwenye maoni yako, kwa sababu hakuna anayejua unachojua wewe, kuhusu wewe binafsi na kile unachotaka.
Jiambie NDIYO kwenye kile hasa unachotaka.
Waache wengine waseme hapana, hayo ni maoni yao, wewe chukua maoni yako ya NDIYO.
Ukawe na siku bora sana yaleo, siku ya kusikiliza NDIYO yako kuliko unavyosikiliza HAPANA ya wengine.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha