Epictetus said, you “should not be satisfied with mere learning, but add practice then training. For as time passes we forget what we learned and end up doing the opposite, and hold opinions the opposite of what we should.”
Siku mpya,
Siku bora,
Siku ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wetu wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UTASAHAU ULICHOJIFUNZA…
Kila unachojifunza, utasahau baada ya muda, kama hutakiweka kwenye matendo.
Akilo zetu haziwezi kushikilia kitu kwenye kumbukumbu kwa muda mrefu.
Hivyo tunajikuta baada ya muda tunafanya tofauti na tulichojifunza na kuamini kinyume kabisa na tulivyojifunza.
Njia pekee ya kukumbuka ulichojifunza ni kukifanyia kazi na baadaye kuwa sehemu ya maisha yako.
Kama hutachukua hatua, kama hutaweka kwenye matendo chochote unachojifunza, haitakuchukua muda kabla hujasahau na kurudi kwenye yale ambayo ni kinyume na ulichojifunza.
Jifunze kisha chukua hatua, ishi yale uliyojifunza, yatengeneze maisha yako kwenda kadiri ya uliyojifunza.
Na kila kitu kipya unachojifunza na kukifurahia, weka kwenye matendo mara moja.
Ni rahisi kukumbuka ulichojifunza, lakini ukishakifanyia kazi, ukishakiweka kwenye matendo, inakuwa tabia. Na tabia ni ngumu sana kusahau au kuvunja. Kwa sababu mwili unajiendesha kwa tabia.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujifunza na kifanyia kazi yale uliyojifunza ili usiyasahau na kujifunza kwako kukakosa maana.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha