Jim Rohn once remarked that “The greatest reward in becoming a millionaire is not the amount of money that you earn. It is the kind of person that you have to become to become a millionaire.”
AMKA Mwanamafanikio,
AMKA kwenye siku hii nyingine nzuri sana kwetu,
Nafasi ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari SIYO MATOKEO, BALI MCHAKATO…
Lengo lolote kubwa unalojiwekea kwenye maisha yako, jua utakachonufaika nacho siyo kufikia lengo hilo, bali mchakato wa kufikia lengo hilo.
Safari nzima ya kufikia lengo kubwa unalopigania ndiyo yenye manufaa kwako.
Ule mchakato mzima ndiyo unaokufundisha na kukutengeneza kuwa mtu bora sana.
Hivyo unapojiwekea lengo kubwa, iwe ni kuwa bilionea au lengo jingine lolote, usiangalie tu yale matokeo ya mwisho, bali angalia mchakato mzima unaokufikisha kwenye matokeo hayo.
Furahia kila hatua unayochukua kuelekea kwenye lengo hilo, maana kila hatua inakufanya wewe kuwa bora zaidi.
Kinachowafanya baadhi ya wanaofanikiwa kukosa furaha ni kuacha kuangalia mchakato na kuangalia matokeo pekee. Hivyo wanapoyafikia matokeo, ndiyo wanajiuliza kuna nini tena?
Lakini unapoangalia mchakato mzima, hata usipopata matokeo unayotazamia, utanufaika sana na machakato.
Jiwekee malengo makubwa sana,
Na kila siku piga hatua kuelekea kwenye malengo hayo,
Huku ukifurahia kila hatua unayopiga,
Kwa sababu kitakachokunufaisha siyo matokeo utakayopata, bali ule mchakato unaokupeleka kwenye matokeo.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kufurahia mchakato mzima wa kufikia malengo yako makubwa.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha