“We are all born for love. It is the principle of existence, and its only end.” — Benjamin Disraeli
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JAWABU LA KILA KITU..
NI UPENDO.
Upendo ndiyo jawabu la kila kitu kwenye maisha yetu.
Kila tunachopitia, kiwe kizuri au kibaya, jawabu lake ni upendo.
Njia pekee ya sisi binadamu kuweza kuwa na maisha bora na kuweza kupiga hatua hapa duniani ni kuwa na upendo.
Upendo ndiyo msingi mkuu wa maisha ya mafanikio.
Upendo ndiyo kitu pekee ambacho kila mtu anaweza kuwa nacho, bila ya kujali yupo kwenye hali gani.
Changamoto nyingi ambazo watu wanapitia, zinaweza kutatuliwa na upendo na hata kama hazitatulikim basi upendo utazifanya zisiwe kikwazo.
Ishi kwa upendo na sambaza upendo.
Jipende wewe mwenyewe, kwa sababu usipojipenda wewe ni vigumu sana kuwapenda wengine.
Wapende wale wanaokuzunguka kwa sababu ndiyo watakaokupa chochote unachotaka kwenye maisha yako.
Na pia penda sana kile unachofanya kwenye maisha yako, iwe ni kazi au biashara, kwa sababu ukishapenda unachofanya, hakitakuwa kigumu tena kwako.
Tumezaliwa kwa upendo, na mafanikio yetu ni matokeo ya upendo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuishi kwa upendo wa hali ya juu, leo na kila siku ya maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha