“How can we learn self-knowledge? Never by taking thought but rather by action. Try to do your duty and you’ll soon discover what you’re like.” — Goethe

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TEKELEZA MAJUKUMU YAKO…
Kama unataka kujijua wewe mwenyewe, tekeleza majukumu yako,
Kama unataka wengine wakujue, tekeleza majukumu yako,
Kama unataka kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako, tekeleza majukumu yako.

Unaweza kufikiri kwa kina,
Unaweza kutafakari,
Unaweza kuwaambia wengine wewe ni nani na wakuchukulieje,
Lakini wao hawatakusikiliza, bali watakuangalia unafanya nini.
Watu watabeba zaidi kile unachofanya na namna unavyokifanya kuliko vile unavyoongea.

Hivyo weka nguvu zako, muda wako na umakini wako kwenye kutekeleza majukumu yako.
Kwa kufanya, utajua maeneo gani unahitaji kuboresha zaidi.
Na kwa kuwa tayari kwenda hatua ya ziada, unajua ni mbali kiasi gani unaweza kwenda.

Kama ukiweka kipaumbele kwenye kutekeleza majukumu yako, hutapata muda wa kusumbuliwa na fikra hasi na hata hofu za wengine. Kwa sababu wewe utakuwa umemezwa na kufanya na siyo hofu za kufikirika.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kutekeleza majukumu yako kwa kipaumbele kikubwa na kupunguza kufikiri na kuongea zaidi kuhusu majukumu yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha