Nietzsche observed, “He who has a why to live for can bear almost any how.”
Siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UNA KWA NINI YA MAISHA YAKO?
Watu wawili, wanaweza kuwa wanaanzia chini kabisa, wanafanya kitu kinachofanana na wote wanakutana na changamoto zinazofanana, lakini mmoja anafanikiwa huku mwingine anashindwa na kukata tamaa.
Je ni nini kinaweza kuwa kinawatofautisha watu hawa?
Wapo watu wanaoonekana kupitia magumu sana, ambayo watu wa nje wanasema anawezaje kuvumilia hivyo, je nini kinawasukuma watu wa aina hiyo?
Kinachowatofautisha wanaofanikiwa sana, na kinachowasukuma wanaovuka changamoto ngumu sana ni KWA NINI YA MAISHA YAO.
Kama alivyoona Fredrick Nietzsche, mtu yeyote mwenye kwa nini ya maisha yale, anaweza kuvuka chochote.
Kwa nini ina msukumo mkubwa sana.
Unapokuwa na sababu ya wewe kuishi, unapokuwa na kitu kinachokuamsha kitandani kila siku,
Unapokuwa na kitu ambacho upo tayari kukifia,
Changamoto yoyote unayokutana nayo haikusumbui, kwa sababu wewe huangalii changamoto, bali unaangalia unapataje unachotaka.
Mtu mmoja amewahi kunukuliwa akisema, nakwenda kupanda mlima mrefu sana, tegemeeni vitu viwili, kuniona kileleni mwa mlima nikishangilia au kunikuta njiani nikiwa nimekufa.
Unafikiri mtu wa aina hii nini kitamzuia?
Rafiki, asubuhi hii tafakari ni nini kinakusukuma kwenye maisha yako,
Jiulize kwa nini yako ni nini.
Nini kinakusukuka kuamka kila siku,
Kipi upo tayari kutesekea na hata kuumia.
Jua kwa nini ya maisha yako na utaweza kuvuka kila aina ya changamoto na kufanikiwa sana.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuitumia kwa nini ya maisha yako kufanya makubwa zaidi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha