“Nothing seems to me more unhappy than someone to whom nothing adverse has ever happened.” – Demetrius
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii mpya na nzuri sana kwetu leo.
Ni nafasi nyingine bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA HUJAKUTANA NA MAGUMU, HUWEZI KUWA NA FURAHA…
Huwa hatupendi kukutana na magumu kwenye maisha yetu, tunatamani maisha yangekwenda kwa unyoofu bila ya changamoto yoyote.
Lakini pia maisha ambayo hayana magumu na changamoto, ni maisha ambayo hayana furaha kuyaishi.
Kwa sababu magumu na changamoto tunazokutana nazo, ndiyo yanafanya maisha yetu yawe na maana.
Magumu na changamoto tunazokutana nazo, ndiyo yanatuwezesha kujijua sisi wenyewe na uwezo mkubwa tulionao.
Magumu na changamoto tunazokutana nazo, ndiyo yanatuwezesha kuwa bora zaidi, kufanya zaidi na kuweza kupiga hatua zaidi.
Maendeleo yoyote tunayoyaona hapa duniani, ni kwa sababu ya magumu na changamoto ambazo watu wamepotia.
Kwa kutatua magumu hayo, ndiyo tunaendelea kupata maendeleo bora kabisa.
Unapokutana na magumu na changamoti, usiumie, usikimbie na wala usitamani yasingekukuta wewe.
Badala yake yaendee magumu hayo, jiandae kuyakabili na jua ukishayavuka, utakuwa bora zaidi kuliko ulivyokuwa kabla.
Angalia miti miwili, mti mmoja umeota sehemu yenye upepo mkali na ukame na mti mwingine umeota sehemu yenye maji mengi na isiyo na upepo kabisa, je ni mti gani utakaokuwa imara zaidi?
Ni ule ulioota kwenye mazingira magumu.
Asili inavifanya vitu vinavyopitia ugumu kuwa bora zaidi,
Na vile visivyopitia ugumu kuwa dhaifu kiasi cha kushindwa kustahimili ugumu wowote.
Furahia unapokutana na magumu na changamoto, kwa sababu unajua utakiwa imara na bora zaidi baada ya kuvuka hayo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukaribisha magumu na changamoto na kuyatumia kuwa bora zaidi.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha