“I will keep constant watch over myself and – most usefully – will put each day up for review… Let us balance life’s books each day.” – Seneca
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TENGENEZA MIZANIA YA MAISHA YAKO KILA SIKU…
Kila siku tunayopata nafasi ya kuwa hai, nafasi ya kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwetu, ni siku ambayo tunapaswa kuitumia vizuri sana.
Kila siku tunapaswa kutengeneza mizania ya maisha yetu, kwa kutafakari kila tulichofanya kwenye siku yetu.
Kila ambacho tumepanga kufanya kwenye siku yetu, tunapaswa kukifanya kama tulivyopanga.
Na mida wetu, kitu ambacho kina thamani zaidi, tunapaswa kuulinda na kuutumia kwa yale ambayo ni muhimu sana kwetu.
Watu wanapoteza maisha yao yote kwa sababu ya kupoteza siku moja moja.
Kama tutakuwa makini na kila siku yetu, kwa kuipangilia vizuri, kujisimamia vizuri kwenye siku husika na pia kutafakari kila mwisho wa siku yetu, itakuwa rahisi kuona wapi tunakosea na kuweza kufanya marekebisho mapema.
Iweke kila siku yako kwenye tafakari na kipimo, tengeneza mizania ya kila siku yako na hii itakusaidia usiyapoteze maisha yako.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kutengeneza mizania ya maisha yako, kulinda muda wako na kufanya yale muhimu.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha