In business (and perhaps in life), you’ve got to have a good reason for what you’re doing. And if you don’t have a good enough reason, you should probably ditch it.
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana kwetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA HUNA SABABU KUU YA KUFANYA, NI BORA UACHE…
Kwa chochote unachofanya kwenye maisha yako rafiki, unapaswa kuwa na sababu kuu ya kufanya.
Sababu kuu ambayo itakuamsha kutoka kitandani asubuhi,
Sababu kuu ambayo itakuwezesha kuvuka magumu na changamoto mbalimbali ambazo lazima utakutana nazo kwenye safari yako.
Kama huna sababu kuu, kama huna sababu ambayo inakusukuma sana, hutaiweza safari unayoianza. Kwa sababu haitakuwa safari rahisi hata kidogo.
Ninaposema sababu kuu, namaanisha sababu ambayo inatoka ndani yako kweli, sababu ambayo haiwezi kurubuniwa na yeyote yule, sababu iliyosimama na haiwezi kutetereshwa na chochote.
Kufanya kwa sababu kila mtu anafanya, au kwa sababu unataka uonekane na wewe unafanya, au kutaka kuwaridhisha watu fulani, siyo sababu sahihi za kufanya, na kadiri unavyoendelea kufanya chochote kwa sababu hizo, unajiumiza wewe mwenyewe.
Kufanya kwa sababu unataka kuacha alama kwenye hii dunia, kwa sababu unajua ndani yako kuna kitu kikubwa unapaswa kutoa, kwa sababu unapenda kuyaona maisha ya wengine na yako yakiwa bora zaidi, ni sababu sahihi kwako kufanya na kila matokeo madogo utakayoyapata yatachochea wewe kupiga hatua zaidi.
Rafiki, leo kaa chini na tafakari hili kwa kina, orodhesha kila unachofanya kwenye maisha yako, kisha oroshesha sababu kuu za kufanya kila unachofanya.
Kama kuna kitu unafanya na huna sababu kuu za kukifanya, acha kukifanya mara moja.
Kwa sababu unapoteza nguvu, unapoteza muda, unapoteza maisha na unajichelewesha kufanya yale ambayo ni muhimu zaidi kwako.
Na ukumbuke, una maisha haya uliyonayo pekee hapa duniani, usiyatapanye hovyo kwa kufanya vitu visivyo muhimu kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kile ambacho una sababu kuu ya kufanya.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha