The Stoics teach us, when we butt up against someone else’s awfulness, to always remember when we ourselves have behaved like that.

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni siku ambayo tuliisubiri kwa shauku kubwa sana,
Siku ambayo jana tulisema kesho tuta….
Kesho yenyewe ndiyo hii sasa, hivyo chondechonde usisime tena kesho nita, bali fanya leo.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KAMA VILE WEWE HUJAWAHI KUKOSEA…
Watu wanapokosea,
Watu wanapofanya tofauti na tunavyotegemea,
Huwa tunastuka na kushangaa, kwa nini wamefanya hivyo, inawezekanaje wakosee au kufanya kisichostahili.
Kwa namna unavyostuka na kushangaa, ni kama vile wewe binafsi hujawahi kukosea, kama vile katika maisha yako yote hujawahi kufanya ambacho hakistahili.

Rafiki, sisi ni binadamu na moja ya udhaifu ambao kila mmoja wetu anao ni kukosea. Wakati mwingine tunakosea tukijua, wakati mwingine tunakosea bila ya kujua, hivyo kukosea ni ubinadamu.
Kwa sababu wewe makosa yako hayaonekani na wengine au kuwadhuru wengine, haikufanyi wewe kuwa mtakatifu sana zaidi ya wengine.
Hivyo usiwe mtu wa kuhukumu sana wengine pale wanapokosea, badala yake waelewe kama binadamu.

Wakati mwingine wape watu nafasi ya kukosea, tegemea kwamba wangekosea, na elewa kwamba kuna mengi yanayoendelea kwenye maisha yao, ambayo yanaweza kuwa yamewavuruga wasiweze kufikiri na kufanya yaliyo sahihi.

Kabla hujakasirishwa na kushtushwa na makosa ya wengine, hebu jiulize kwanza wewe mwenyewe kuhusu makosa ambayo umekuwa unayafanya.
Kwa kufikiri hivi hakukufanyi ukubali kila makosa ya wengine, wala hakukufanyi uwaachie wengine wakosee wanavyotaka, ila inakuleta kwenye uhalisia wa sisi binadamu.
Bado utaendelea kuwataka watu wafanye kwa ubora wa hali ya juu sana, kadiri ya uwezo wao.
Bado utawataka watu wawe makini zaidi na kujali zaidi.
Lakini pale wanapofanya kinyume, isikushangaze sana na kuona kama ni kitu kigeni mno, siyo, ni kama ambavyo nawe pia umekuwa unakosea.

Kwa kufikiri na kuchukulia mambo hivyo pia inakuweka kwenye nafasi nzuri ya kuweza kuchukua hatua sahihi pale kinapotokea kile ambacho hukutegemea kitokee.
Wengi huwa wanaweka mategemeo yao yote kwa asilimia 100 kwenye kile wanachotegemea wengine wafanye, hivyo wasipofanya, wanakwama kabisa.
Unapowapa wengine nafasi ya kukosea, unajipanga kwa njia mbadala pale kinapotokea usichotegemea.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwapa wengine nafasi ya kukosea na kutokujiweka kwenye nafasi ya kukwama pale wengine wanapokosea.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha