The Stoic must cultivate their own high standards, their own strong opinions about what is right and good and important. This is what they need to use to evaluate reality. Other people’s opinions? We need to stop caring about them.
Hongera sana mwanamafanikio kwa nafasi hii nyingine nzuri sana kwetu.
Ni fursa ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari SIMAMA KWA MIGUU YAKO MWENYEWE…
Kadiri tunavyokwenda, ndivyo ambavyo watu wengi wanashindwa kusimama kwa miguu yao wenyewe.
Watu wengi hawajajiwekea viwango vya hali ya juu sana wanavyoviishi, badala yake wanaangalia wengine wanafanya nini na wao wanafanya.
Watu wengi hawana msingi wao wa maoni wanayoyasimamia, kuhusu kipi kibaya, kipi kizuri na kipi muhimu, badala yake wanaangalia wapi penye wengi na kujiunga na hao wengi.
Watu wengi hawana msimamo kwenye maisha, wanayumbishwa kama upepo na maoni ya kila mtu. Wanayapa uzito maoni ya kila mtu na mwisho wanabaki wasijue kipi cha kufanya.
Mfano mtu anapata hamasa ya kuchukua hatua ili afanikiwe, wengine wanamwamboa usijisumbue huwezi kufanikiwa, anawasikiliza na kukubaliana nao.
Mtu anajiambia sasa naanza kuweka umakini kwenye fedha zangu, anajitokeza mtu ambaye hata fedha hana, anamwambia fedha siyo kila kitu, anakubaliana naye na anaacha kuweka umakini kwenye fedha.
Rafiki, kama unataka kutoboa kwenye haya maisha, kama unataka kufika kule unakotaka kufika, lazima uchore mstari wa wapi unasimama na kipi unachosimamia. Na kila mtu aelewe kabisa kwamba unasimama wapi.
Ukishachora mstari wako, wapo wengi watakaokubeza na kukukatisha tamaa, lakini hupaswi kuwasikiliza hata kidogo, kwa sababu watu watakaoanza kuhangaika na maisha yako, ni wale ambao hawana maisha yao. Kama wangekuwa na maisha yao, wangekuwa bize sana wasingejua hata ni nini kinaendelea kwenye maisha yako.
Rafiki, jifunze kusimama kwa miguu yako mwenyewe,
Usitegemee kukubalika na kila mtu ndiyo uchukie hatua,
Usisubiri mpaka kila mtu akushangilie ndiyo uone umefanya vizuri,
Weka viwango vyako vya hali ya juu sana na viishi hivyo.
Jiambie ni yapi sahihim yapi siyo sahihi na yapi ni muhimu zaidi kwako.
Kisha simamia hilo.
Kama kitu siyo sahihi, hata kama kila mtu anafanya, haikibadilishi, kitabaki kuwa siyo sahihi.
Kama kitu siyo muhimu zaidi, hata kama mtu anakusukuma kwa namna gani ufanye, kitabaki kuwa siyo muhimu.
Jifunze kusimama kwa miguu yako mwenyewe na maisha yatakuwa rahisi kwako, japo hayataenda kwa urahisi.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kusimama kwa miguu yako mwenyewe, siku ya kuishi kwa viwango vya hali ya juu sana ulivyojiwekea mwenyewe, siku ya kusimamia kilicho sahihi na kufanya yaliyo muhimu pekee.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha