“The new basic principle is that in order to learn to avoid making mistakes, we must learn from our mistakes. To cover up mistakes is, therefore, the greatest intellectual sin.” — Karl Popper

Siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni nafasi bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIFICHE MAKOSA UNAYOFANYA.
Kitu kinachowazuia watu wengi kujifunza ni kutokupenda kufanya makosa.
Hivyo wengi huacha kabisa kufanya pale wanapoona upo uwezekano wa kufanya makosa.
Wengine wanafanya makosa, ila wanayaficha, hawataki yaonekane na wengine.

Rafiki, hakuna ubaya wowote kwenye kufanya makosa, ndiyo njia ya kujifunza hiyo.
Unapofanya makosa na ukatafakari nini kimechangia, unapata njia bora zaidi ya kufanya unachofanya na kuepuka kurudia tena makosa hayo.

Lakini kama utakwepa kufanya ili usikosee, hutajifunza chochote kikubwa.
Kadhalika kama utakosea halafu ukaficha makosa hayo, unajidanganya tu wewe mwenyewe.

Tunajifunza vizuri kupitia makosa tuliyofanya, hivyo ni vyema kila mmoja wetu akawa tayari kufanya makosa zaidi na kuyokuyaficha au kuyakimbia.
Hakuna mtu atakayekucheka wewe kwa sababu umekosea kitu fulani, kwani kila mtu anakosea.
Na kingine kinachopaswa kukupa nguvu ni kwamba hakuna mtu anayeyafuatilia maisha yako kama unavyofikiri.
Wengi wanapambana na maisha yao wenyewe na hawajui hata ni makosa gani unafanya.

Fanya makosa mapema ili ujifunze mapema, kuliko kuyakwepa au kuyaficha, kitu ambacho kitakuwa mzigo zaidi kwako baadaye.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kujifunza kupitia makosa ambayo unayafanya.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha