“Time is infinitely more precious than money, and there is nothing common between them. You cannot accumulate time, you cannot borrow time, you can never tell how much time you have left in the bank of life. Time is life.”

Siku mpya,
Siku bora na ya kipekee sana kwetu,
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ilo kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari MUDA NI MAISHA…
Huwa tunapenda kusema muda ni fedha,
Lakini hili siyo sahihi,
Hakuna hsawa wowote kati ya muda na fedha.
Unaweza kuweka fedha benki, lakini huwezi kuweka muda kwa ajili ya baadaye.
Unaweza kukopa fedha lakini huwezi kukopa muda.
Ukipoteza fedha unaweza kupata nyingine, lakini ukipoteza muda huupati tena.
Unaweza kujua ni kiasi gani cha fedha umebaki nacho lakini huwezi kujua kiasi gani cha muda umebaki nacho kwenye maisha.
Hivyo muda una thamani kubwa kuliko fedha.

Kitu pekee kinachoweza kuwa sawa na muda ni maisha.
Muda ndiyo maisha yenyewe.
Ukipoteza muda umepoteza maisha yako mwenyewe.
Ukitumia vizuri muda wako, unakuwa na maisha bora kwako.

Linda sana muda wako kwa sababu hayo ndiyo maisha yako.
Na unapokuwa unapoteza muda usiseme napoteza muda hapa, bali sema napoteza maisha hapa.
Kwa sababu kinachokupita ni maisha ambayo ungeweza kuyaishi kwa muda uliopoteza.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutunza sana muda wako kwa sababu hayo ndiyo maisha yako.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha