“In some way, suffering ceases to be suffering at the moment it finds a meaning, such as the meaning of a sacrifice.” – Victor Frankl
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MATESO NA MAANA…
Ili kufikia mafanikio makubwa unayotarajia, kuna wakati utapitia mateso makali.
Na hapa kwenye mateso, ndipo wengi wanapokata tamaa na kuacha kufanya walichopanga kufanya.
Mateso ni magumu na yanaumiza, kama mtu huna maana kubwa inayokusukuma, maana inayozidi mateso yote, hutaweza kuvumilianna kuvuka mateso hayo.
Mateso yanaacha kuwa mateso pale yanapokutana na maana kubwa.
Pale unapokuwa na KWA NINI kubwa inayokusukuma kufanya makubwa, hutayaona mateso, wewe utaona ni njia ya kufika unakotaka kufika.
Wanaokuzunguka, ambak hawajui maana kubwa uliyonayo wataona unajitesa, watakushauri usijitese, urudi kwenye mambo ya kawaida ambayo wao wanafanya. Na ukiwasikiliza hao, huwezi kupiga hatua.
Hatua ya kwanza kabisa ya kufanikiwa ni kuwa na maana kubwa ya kwa nini unataka unachotaka, maana ambayo itayashinda mateso yoyote utakayokutana nayo kwenye safari yako.
Bila maana hiyo kubwa, safari itakuwa ngumu sana kwako.
Kila wakati hakikisha una jibu la swali hili; kwa nini niteseke na magumunwakati kuna mengine rahisi kufanya? Ukiwa na jibu la swalo hili, unapokutana na ugumu na mateso havitakuteteresha.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na maana kubwa ya kwa nini uteseke ili kupata mafanikio makubwa unayoyatafuta.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha