Marcus Aurelius’s admonishment to himself, “Just that you do the right thing. The rest doesn’t matter. Cold or warm. Tired or well-rested. Despised or honored.”

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari FANYA KILICHO SAHIHI…
Mara nyingi kwenye maisha yako utajikuta njia panda,
Utakuwa njia panda ya kufanya kilicho sahihi au kufanya kilicho rahisi.
Mara zote na katika hali zote, fanya kilicho sahihi.
Kilicho sahihi huwa ni kigumu kufanya na matokeo yake huchelewe, lakinj ndiyo kitu sahihi kufanya na chenye matokeo bora.

Mara zote fanya kilicho sahihi, bila ya kujali wengine wanafanya nini au kusema nini.
Mara zote fanya kilicho sahihi bila ya kujali wewe upo kwenye hali gani.
Ukitafuta sababu za kutokufanya kilicho sahihi, utazipata nyingibna zenye ushawishi,
Umeonewa, dunia haina usawa, umechoka, mazingira hayaruhusu, kila mtu anafanya, zote hizo ni sababu ambazo zinaweza kuonekana ni nzuri sana, lakini bado hazifanyi kisicho sahihi kuwa sahihi.

Fanya kilicho sahihi mara zote, siyo kwa sababu unaonekana na wengine, na wala siyo kwa sababu utawafurahisha wengine, bali kwa sababu ndiyo kitu sahihi kufanya.
Ukishafanya kilicho sahihi, wewe unachosubiria ni matokeo bora. Huna haja ya kuwa na hofu kwamba kuna vitu vya tofauti vitajulikana baadaye. Hutahitaji kupoteza nguvu yoyote kwenye kuficha chochote.
Unapofanya kilicho sahihi, mara zote unakuwa huru na maisha yako na nguvu zako zoye unazipeleka kufanya hale muhimu.

Ili uweze kufanya kilicho sahihi mara zote, lazima uwe na msingi wa maisha ambao unausimamia bila ya kutetereka. Bila ya kuwa na msingi wa aina hii, dunia itakujaribu mno na hutaweza kustahimili majaribu hayo. Ukiwa na msingi na ukiufuata, mambo yako yatakuwa bora sana.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kike kilicho sahihi, kwa sababu ndiyo kitu sahihi kufanya.
#Fanya #HakunaSababu #NiLeoTu #IngiaMzimaMzima #AnzaNaHatuaMoja #MafanikioNiHakiYako #NidhamuMsingi #WhatEverItTakes #WachaManenoWekaKazi #SkinInTheGame #OwnTheDayOwnYourLife #UsileteSababuLetaMatokeo #MudaNiSasa

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha