“For one human being to love another human being: that is perhaps the most difficult task that has been entrusted to us, the ultimate task, the final test and proof, the work for which all other work is merely preparation.” — Rainer Maria Rilke

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari JUKUMU GUMU KABISA TULILOPEWA…
Kama lipo jukumu gumu kabisa ambalo sisi binadamu tumepewa, basi ni jukumu ka kupendana sisi wenyewe.
Mtu mmoja kumpenda mwingine ndiyo jukumu kubwa na gumu zaidi ambalo tumepewa.
Tena pale unapopaswa kumpenda mwingine bila ya masharti yoyote, kumpenda kama alivyo, ni jukumu gumu, lakini lenye matokeo mazuri sana.

Kitu pekee kitakachotuwezesha sisi binadamu kuendelea kudumu na kufanikiwa ni upendo baina yetu.
Tunapopendana kama binadamu na kujaliana, tunafanya mambo ambayo ni bora kwa kila mmoja wetu.
Tunapowapenda wengine hatuwezi kiwaibia, hatuwezi kuwadhulumu na wala hatuwezi kufanya chochote cha kuwaumiza.

Tunapowapenda na kuwajali wengine, tunajituma kwa kufanya kile ambacho ni bora mara zote, tunakwenda hatua ya ziada na kila tunachofanya kinakuwa kile ambacho kinamchango mzuri kwa wengine.

Jukumu letu kuu ni kupendana kama binadamu, mengine yote tunayofanya ni maandalizi ya kutekeleza jukumu hili kuu.
Jipende wewe mwenyewe na wapende wengine, hiyo ndiyo njia pekee ya wewe kukamilisha utu wako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na upendo usio na masharti kwa wengine, siku ya kuwapenda wengine kama watu na kama jukumu lako kuu.
#SambazaUpendo, #JipendeMwenyewe, #WapendeWengine, #MaishaNiUpendo

Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha