“A person who doesn’t know what the universe is, doesn’t know where they are. A person who doesn’t know their purpose in life doesn’t know who they are or what the universe is. A person who doesn’t know any one of these things doesn’t know why they are here. So what to make of people who seek or avoid the praise of those who have no knowledge of where or who they are?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.52

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari WAPI, NANI, NINI NA KWA NINI..

Marcus anatuambia mtu asiyejua ulimwengi ni nini, hajui yupo wapi.

Mtu asiyejua kusudi lake kwenye maisha hajijui yeye ni nani na yupo kwenye ulimwengu gani.

Na mtu asiyejua ulimwengu na kutokujijua yeye mwenyewe, hajui kwa nini yupo hapa ulimwenguni.

Rafiki, ili maisha yetu yaweze kuwa bora, hatuwezi kukwepa kuwa na majibu ya maswali haya muhimu.

Wewe ni nani? Hili ni swali ambalo siyo la kuuliza jina lako, bali la kujieleza wewe kama mtu ambaye uko hapa duniani.

Hapa uko wapi? Ni muhimu kuujua ulimwengu ambao upo.

Kwa nini uko hapa? Ni lazima ujue kusudi la wewe kuwa hapa duniani, hujafika hapa kwa bahati tu, bali kuna kusudi lipo ndani yako, lazima ulijue na kuliishi ndiyo maisha yako yakamilike.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kujua uko wapi, wewe ni nani na unafanya nini hapa.

#JuaUlipo, #JuaKusudi, #AchaAlama

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

http://www.amkamtanzania.com/kocha