“The proper work of the mind is the exercise of choice, refusal, yearning, repulsion, preparation, purpose, and assent. What then can pollute and clog the mind’s proper functioning? Nothing but its own corrupt decisions.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.11.6–7

Hongera mwanamafanikio kwa fursa hii nyingine nzuri sana ya leo.

Ni nafasi nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KAZI SABA ZA AKILI…

Majibu na suluhisho la kila tunalopitia kwenye maisha yetu yanapatikana ndani ya akili zetu.

Akili tulizonazo zina uwezo wa kufanya makubwa sana kama tutazitumia vizuri.

Epictetus anatukumbusha kazi saba za akili zetu, ambazo ni kama ifuatavyo!

KUCHAGUA kufikiri na kufanya kilicho sahihi.

KUKATAA majaribu.

KUTAMANI kuwa bora zaidi.

KUONDOKANA na uhasi na ushawishi mbaya wa yasiyo kweli.

KUJIANDAA kwa yale yanayoweza kutokea mbele yetu.

KUSUDI kuwa na msingi unaoendesha maisha yetu.

KUKUBALI kuwa huru na kujua kilicho ndani na nje ya uwezo wetu na kukubali yale yaliyo nje ya uwezo wetu.

Hizi ndizo kazi saba za akili zetu, tunapaswa kuzifanya kwa usahihi na kuachana na mengine ambayo hayana umuhimu kwetu. Kwa sababu yale yasiyo muhimu yanakuwa uchafu kwa akili zetu.

Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya kuitumia akili yako kufanya yale ambayo ni sahihi kwako.

#CHAGUAsahihi, #KATAAmajaribu, #TAMANIubora, #ONDOKANAuhasi, #JIANDAEkwayajayo, #KUSUDIlamaisha, #KUBALIkuwahuru.

Wako Rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

http://www.amkamtanzania.com/kocha