Rafiki yangu mpendwa,

Heri ya mwaka mpya 2019.

Huu unapaswa kuwa mwaka wa tofauti na wa kipekee sana kwako, siyo tu kwa maneno, bali kwa matendo pia.

Mwaka huu unapaswa kuufanya mwaka wa kuchukua hatua badala ya kuufanya mwaka wa kujipanga na kujiandaa.

Umeshajipanga vya kutosha, umeshajiandaa vya kutosha na sasa nakuambia upo tayari kuanza na anzia hapo ulipo sasa, kwa chochote ulichonacho sasa.

Katika kukuhakikishia unauanza mwaka huu wa vitendo, huku ukiwa na maarifa sahihi kwako nimekuandalia zawadi ya VITABU VYA MAFANIKIO.

Katika zawadi hii, nakwenda kukupa bure kabisa nusu ya vitabu ambavyo nimeandika. Mpaka sasa nimeandika vitabu nane, na ninataka kukupa nusu ya vitabu hivyo bure kabisa ili mwaka huu 2019 uuanze ukiwa na silaha kamili za kushinda.

095a5b996f7db11bfe3b1d93a17b444b.0vitabu softcopy

Vitabu nane ninavyokwenda kukupa kama zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu 25 kwa nini unaendelea kuwa masikini. Bei ya hikii ni tsh elfu 5 (5,000/=). Ndani ya kitabu hiki utajifunza sababu 25 zinazokuweka kwenye umasikini na jinsi ya kuondokana nazo ili uwe na maisha bora.
  2. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA; Maandalizi na njia bora ya kunufaika na mabadiliko kwenye maisha, kazi na biashara. Bei yake tsh elfu 5 (5,000/=). Kitabu hiki kinakuandaa na mabadiliko yanayoendelea kutokea kwa kasi na kuhakikisha unakuwa mbele kabla mabadiliko hayajakuacha nyuma.
  3. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG, Jiajiri na utajirike kupitia mtandao wa intaneti. Bei yake elfu 10 (10,000/=). Kama una simu janja (smartphone) na unaweka bando kila siku lakini huingizi hata mia tano kutoka kwenye mtandao unajinyima fursa nzuri ya kutengeneza kipato. Soma kitabu hiki upate maarifa ya jinsi ya kuingia kipato kwa kutumia simu yako janja.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, TOLEO LA KWANZA 2016; Nidhamu, Uadilifu Na Kujituma. Bei yake ni tsh elfu 10 (10,000/=). Maisha yenye mafanikio ni maisha ambayo mtu unaishi kwa msingi. Msingi mkuu wa maisha ya mafanikio ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, jifunze zaidi kuhusu msingi huu kwenye kitabu cha kurasa za maisha ya mafanikio.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA; Anzisha na kuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Bei yake tsh elfu 10 (10,000/=). Kama umeajiriwa na kipato chako hakikutoshelezi kuwa na maisha unayotaka, unaweza kutengeneza kipato cha ziada huku ukiendelea na ajira yako. Kitabu cha biashara ndani ya ajira kitakupa maarifa hayo.
  6. MIMI NI MSHINDI; Ahadi yangu na nafsi yangu. Bei tsh elfu 10 (10,000/=). Ndani yako, upo uwezo mkubwa wa kukuwezesha kupata chochote unachotaka kufanya. Unachohitaji ni kujua uwezo huo na kuutumia. Kitabu cha mimi ni mshindi kinakuwezesha kujua uwezo mkubwa uliopo ndani yako.
  7. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU; dhibiti muda wako ili uweze kufanya zaidi. Bei yake tsh elfu 5 (5,000/=). Kama kuna kitu unataka kufanya kwenye maisha yako lakini unajiambia huna muda, unajidanganya, muda unao mwingi sana. Kitabu cha pata masaa mawili ya ziada kinakuwezesha kupata masaa mawili hata kama unajiona upo bize kiasi gani.
  8. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING); Miliki biashara kubwa kwa kuanza na mtaji kidogo. Bei tsh elfu 5 (5,000/=). Kama kuna watu wako wa karibu wanakusumbua sana kuhusu biashara ya mtandao, kila wanavyokueleza huwaelewi na unaona kama ni utapeli, unajinyima fursa. Ijue misingi ya biashara hii na kujua hatua sahihi za kufanikiwa kupitia biashara hii. Kitabu ijue biashara ya mtandao kitakusaidia sana kwenye hilo.

Rafiki, ukijumlisha bei za vitabu hivyo sita unapata shilingi elfu sitini (60,000), ambayo ndiyo gharama ya kupata vitabu vyote nane nilivyoandika mpaka sasa, kwa njia ya softcopy ambapo unatumiwa kwa email.

Lakini wewe rafiki yangu nimeahidi kukupa zawadi ya kuanza mwaka mpya 2019 na hivyo nakupa bure nusu ya vitabu hivyo nane. Yaani unapata bure kabisa vitabu vinne. Unachopaswa kufanya ni kulipa nusu ya jumla ya gharama ya vitabu hivyo na utapata vitabu vyote nane. Yaani ni sawa na kulipia vitabu vinne na vingine vinne ukapata bure.

Kupata zawadi hii, tuma fedha tsh 30,000/= kwa namba 0755 953 887 au 0717 396 253 (majina AMANI MAKIRITA) kisha nitumie ujumbe kwenye moja ya namba hizo wenye maneno zawadi ya vitabu ukiwa umeambatanisha na email yako kisha nitakutumia vitabu hivyo nane kwenye email yako.

MUHIMU; vitabu hivyo vipo kwa mfumo wa softcopy pekee na vinatumwa kwa email tu. Chukua hatua sasa ili kupata zawadi hiyo ya vitabu na uuanze mwaka wako kwa mafanikio makubwa.

Kama unahitaji vitabu vichache kati ya hivyo, unaweza kulipia vile unavyochagua kwa bei zake zilizooneshwa hapo juu. Ukatuma fedha na majina ya vitabu unavyotaka kisha ukatumiwa.

Zawadi ya punguzo ni kama utachukua vyote nane, ukichukua pungufu utalipa kwa bei kamili ya kila kitabu.

Karibu sana rafiki yangu, sitaki mwaka 2019 ukawe mwaka wa kawaida kwako, nataka ukawe mwaka ambao utaacha alama kubwa kwenye maisha yako. Hivyo uanze mwaka huu na zawadi hii ya kipekee kwako.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA www.kisimachamaarifa.co.tz/kujiandikisha

Kupata huduma za Ukocha; www.kisimachamaarifa.co.tz/kocha