Pale ambapo tunahitaji kufanya kitu kikubwa ambacho kinahitaji muda mrefu ili kuona matokeo yake, huwa tunasita na kuona muda tunaopaswa kuweka ni mrefu sana.
Mfano ni pale mtu anapoona fursa ya kuingia kwenye biashara, lakini ambayo itamhitaji muda kujenga misingi ili iweze kumlipa baadaye, labda miaka mitatu ijayo.
Kwa kuona miaka mitatu, wengi wanasita kuchukua hatua kwa kuona muda ni mrefu.
Lakini ukweli ni kwamba, huo muda utapita tu, iwe umechukua hatua au la. Miaka mitatu itapita tu, iwe umechagua kufanya au kuacha.
Na wala haitakuwa mirefu kama ulivyofikiri, kufumba na kufumbua miaka mitatu itakuwa imeisha.
Sasa kitakachokuumiza sana baada ya miaka mitatu kuisha ni ukweli kwamba hukuchukua hatua, utakumbuka na kujutia hilo mara zote.
Hivyo rafiki, kila wakati unaposita kufanya maamuzi kwa sababu ya muda jikumbushe hili, huo muda unaouhofia utapita tu, na utakachobaki nacho baada ya muda kupita ni maumivu makali.
Muda haukusubiri mpaka wewe uwe tayari, muda hausubiri mpaka wewe uanze, muda unaendelea kwenda. Hivyo wakati bora kabisa kwako kuanza kitu ilikuwa jana, wakati mwingine mzuri ni leo na wakati wa kujidanganya ni kesho.
Chochote muhimu unachotaka kufanya, anza leo na siku nyingi zijazo utajishukuru sana kwa kuanza leo hii. Muda hautakusubiri, hivyo chukua hatua sasa.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante sana kocha muda usivkwamishe kutokuchukua hatua ni leo tu na jana kesho si salama
LikeLike
Karibu Hendry
LikeLike