“Some things are in our control, while others are not. We control our opinion, choice, desire, aversion, and, in a word, everything of our own doing. We don’t control our body, property, reputation, position, and, in a word, everything not of our own doing. Even more, the things in our control are by nature free, unhindered, and unobstructed, while those not in our control are weak, slavish, can be hindered, and are not our own.”
—EPICTETUS, ENCHIRIDION, 1.1–2
Tumeipata nafasi nyingine nzuri sana kwetu rafiki,
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa TATUA, AMUA NA ONGOZA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KILICHO NDANI YA UWEZO WETU NA NJE YA UWEZO WETU…
Katika mambo mengi ambayo yanatokea kwenye maisha yetu, kuna ambayo yapo ndani ya uwezo wetu na tunaweza kuyaathiri. Haya ni yale ambayo yanaanzia ndani yetu kama fikra zetu, maoni yetu, uchaguzi wetu, tamaa zetu na mengine ya ndani.
Pia kuna mambo ambayo yapo nje ya uwezo wetu, ambayo hatuna uwezo wa kuyaathiri. Haya ni mambo yanayotokea nje yetu, kama maoni ya wengine, tabia za wengine, sifa zetu, matendo ya wengine na mengine ya nje.
Ili kuwa na maisha bora, tunapaswa kujua yaliyo ndani ya uwezo wetu na kuyafanyia kazi na yale yaliyo nje ya uwezo wetu tuyapokee kama yalivyo na kukubaliana nayo.
Kujaribu kubadili mambo yaliyo nje ya uwezo wako ni kujiumiza na kujiandaa kushindwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukazana na yaliyo ndani ya uwezo wako na kukubali yaliyo nje ya uwezo wako.
#UpachaWaUdhibiti, #SumbukaNaYaNdani, #KubaliYaNje
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,