Unapokutana na hali ya kutokuwa na uhakika, ambayo inajenga hofu ndani yako, hatua sahihi unayopaswa kuchukua ni kusonga mbele, kuendelea na uliyopanga kufanya na siyo kuacha.
Unapaswa kugeuza kila hofu unayokutana nayo kuwa ukuaji, ifanye hofu iwe sababu ya wewe kupiga hatua zaidi. Kwa sababu kama wote tunavyojua, dawa ya hofu ni kuchukua hatua.
Nenda kafanye kile kinachokupa hofu, na kifanye kwa kujituma na kuweka juhudi zaidi ya ulivyozoea kuweka. Nenda mbele kuhakikisha unaiangusha hofu na kufanya kile muhimu.
Kila unapokutana na hofu, jua hapo ndipo penye uelekeo sahihi, kwa sababu hofu hiyo imewazuia wengi na kama wewe utaishinda, utapata kile ambacho wengi wamekikosa.
Geuza kila hofu yako kuwa ukuaji na utaweza kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante sana umenipa ujasiri kuna kitu kilitaka kunipa hofu lakin ngoja nikifanye
LikeLike
Vizuri sana,
Chukua hatua na hofu yenyewe itakimbia.
Kila la kheri.
LikeLike