“The essence of good is a certain kind of reasoned choice; just as the essence of evil is another kind. What about externals, then? They are only the raw material for our reasoned choice, which finds its own good or evil in working with them. How will it find the good? Not by marveling at the material! For if judgments about the material are straight that makes our choices good, but if those judgments are twisted, our choices turn bad.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.29.1–3
Tumeipata nafasi nyingine nzuri sana kwetu rafiki,
Nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuishi leo kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA. Kwa njia hii tutaweza kupiga hatua kubwa leo kuelekea mafanikio makubwa.
Asubuhi ya leo tutafakari KAMA UNATAKA KUWA NA UTULIVU…
Maisha yana changamoto na misukosuko mingi. Kila wakati kuna kitu kinachokuwa kinaendelea, ambacho hukitegemea kiwe hivyo.
Hivyo kusubiri mpaka nje kutulie ndiyo uwe na maisha ya utulivu utakuwa unajidanganya na kujichelewesha, maana nje hapatatulia.
Kama unataka utulivu kwenye maisha, unaanzia ndani yako, ndani ya fikra zako. Ni pale unapotengeneza fikra za utulivu ndiyo unaleta utulivu kwenye maisha yako. Haijalishi nini kinaendelea nje, kizuri au kibaya, utulivu unaanzia kwenye fikra tunazoruhusu zitawale akili zetu.
Nenda katengeneza fikra za utulivu leo ili uweze kuwa na maisha tulivu, maisha ya kufanya mazuri hata kama umezungukwa na mabaya.
Siku yako ya leo ikawe bora sana, iwe siku ya kutawala fikra zako na kutengeneza utulivu ndani yako.
#UtulivuUpoNdani, #TawalaFikraZako, #UsiyumbishweNaYaNje
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,