“For if a person shifts their caution to their own reasoned choices and the acts of those choices, they will at the same time gain the will to avoid, but if they shift their caution away from their own reasoned choices to things not under their control, seeking to avoid what is controlled by others, they will then be agitated, fearful, and unstable.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.1.12

Tumepata nafasi nyingine nzuri sana ya kuiona siku hii ya leo.

Ni siku ambayo ipo mikononi mwetu, tunao uwezo wa kuitumia vizuri siku hii na kufanya makubwa au tukaipoteza kwa kufanya yasiyo muhimu.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KAMA UNATAKA KUKOSA UTULIVU…

Kama unataka kukosa utulivu kwenye maisha yako, huhitaji hata kwenda mbali na ulipo sasa. Tena wakati mwingine huhitaji hata kifanya kituncha tofauti.

Kama unataka kukosa utulivu, wewe acha kufikiria mambo yako na anza kufikiria mambo ya wengine. Acha kuhangaika na yale yaliyopo ndani ya uwezo wako na anza kuhangaika na yaliyo nje ya uwezo wako.

Kwa maana maisha yetu ni matokeo ya machaguo yetu, na uchaguzi upo ndani ya uwezo wetu.

Chagua kufikiria yale yanayokuhusu na yaliyo ndani ya uwezo wako na upate utulivu. Au chagua kufikiria yale yanayohusu wengine na yaliyo nje ya uwezo wako na ukose utulivu.

Naamini hakuna anayeianza siku yake kwa kudhamiria kukosa utulivu kwenye siku hiyo, ila wengi huteleza na kuanza kusumbuka na mambo yaliyo nje ya uwezo wao. Epuka sana hili.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuhangaika na yaliyo ndani ya uwezo wako na kuachana na yaliyo nje ya uwezo wako.

#UtulivuUpoNdani #HangaikaNaYako #UpachaWaUdhibiti

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

http://www.amkamtanzania.com/kocha