“So in the majority of other things, we address circumstances not in accordance with the right assumptions, but mostly by following wretched habit. Since all that I’ve said is the case, the person in training must seek to rise above, so as to stop seeking out pleasure and steering away from pain; to stop clinging to living and abhorring death; and in the case of property and money, to stop valuing receiving over giving.”
—MUSONIUS RUFUS, LECTURES, 6.25.5–11
Tunayo siku nyingine mpya na ya kipekee sana mbele yetu.
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya upendeleo kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Tunaiendea siku hii kwa msingi wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA ambapo tutaweza kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari USIFANYE CHOCHOTE KWA MAZOEA…
Mara nyingi tumekuwa tunafanya vitu kwenye maisha yetu siyo kwa sababu ndiyo namna bora ya kufanya, au tumefikiri vyema.
Bali huwa tunafanya kwa mazoea, kwa sababu ndivyo ambavyo tumekuwa tunafanya mara zote, kwa sababu ndiyo tulivyozoea kufanya.
Hata maisha yetu, tunekuwa tunayaendesha kwa mazoea, tunafanya yale ambayo tumezoea kufanya mara zote na yanayofanywa na wengi na siyo yaliyo bora kwetu kufanya.
Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kuishi kwa mazoea na kufanya mambo kwa mazoea.
Mazoea ndiyo yanayoleta kila aina ya matatizo na changamoto.
Kwa sababu tukishazoea kitu, tunaacha kufikiri na kufanya leo kama tulivyofanya jana.
Mazoea kwenye maisha yanapelekea watu kurudia yale yale ambayo wamekuwa wanafanya kila siku na kujiingiza kwenye changamoto kubwa.
Mazoea kwenye kazi yanapelekea wengi kuzichoka kazi zao na kutokukua zaidi, hili hupelekea hata watu kuzikosa kazi hizo.
Mazoea kwenye biashara yanatoa mwanya kwa watu kuingia na kuleta ushindani mkali kwako, kitu kitakachokuondoa kwenye biashara.
Kazana sana kuondokana na mazoea, kwa kila unachofanya, jiulize je hii ndiyo namna bora kabisa ya kufanya au ndivyo nilivyozoea kufanya? Mara zote fanya kwa namna bora na siyo kwa mazoea.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kila kitu kwa namna bora na kwa kufikiri badala ya kufanya kwa mazoea.
#MazoeaMabaya, #JaribuVituVipya, #EpukaKundiLaWengi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha