“Pass through this brief patch of time in harmony with nature, and come to your final resting place gracefully, just as a ripened olive might drop, praising the earth that nourished it and grateful to the tree that gave it growth.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 4.48.2

Siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni fursa nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari; IONE DUNIA KAMA MSHAIRI NA KAMA MSANII…
Marcus Aurelius anatukumbusha jinsi ambavyo tuna muda mfupi sana hapa duniani.
Na anatushauri tuishi muda huu mfupi kwa maisha yanayofuata kanuni za asili ili tunaoofika mwisho, uwe mwisho mwema na wa neema.
Kama ambavyo mzeituni uliokomaa unadondoka kutoka kwenye mti wake, unaitukuza dunia ambayo imeulisha na kushukuru mti ambao uneuwezesha kukua.

Vipo vitu vidogo vidogo sana ambavyo vinatokea kwenye maisha yetu ya kila siku, ambavyo ni rahisi kuvizoea na kuvisahau, lakini ni vitu muhimu sana.
Unahitaji kuwa na jicho la mshairi na msanii kuweza kuona vitu hivyo vidogo vidogo na kuvipa thamani inayostahili.
Thamini kila kinachotokea kwenye maisha yako hata kama ni kidogo kiasi gani, shukuru kwa kila jambo hata kama ni jambo dogo mno.

Maisha uliyonayo ni haya pekee, yatumie sasa wakati bado unayo.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuthamini kila eneo la maisha yako na kila hatua unayopiga.
#ThaminiKilaJambo, #ShukuruKwaKilaJambo #MaishaNdiyoHaya.

Wako Rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha