Mpendwa rafiki,
Tunao muda mchache wa kufanya mambo muhimu tu na siyo kufanya kila kitu, binadamu tunaoishi karne ya ishirini na moja tumekabiliwa na changamoto nyingi sana. tumekuwa tunaishi katika dunia yenye kelele nyingi sana na kama hauko makini katika zama hizi ndiyo mwanzo wa kupotea.
Huwa nashangaa sana kuona mtu anapata muda wa kufuatilia mambo ambayo siyo muhimu na hayamwingizii hata fedha. Mtu anayejitambua na anajua amekuja kufanya nini duniani na ana ndoto yake kubwa anayoishi kila siku sidhani kama ataweza kupoteza muda wake kwa mambo ya kijinga wakati ana mambo ya kufanya muhimu.
Watu wengi hawajajitambua kwa sababu kujitambua nayo ni zawadi kutoka kwa Mungu, kama umejitambua unapata wapi muda wa kujisumbua na vitu ambavyo havina mchango chanya kwako?
Mtu pekee unayepaswa kumfuatilia mwaka 2019 ni wewe mwenyewe na siyo mtu mwingine. Kama unataka kupata utulivu wa akili katika zama hizi ishi kufuatilia mambo yako, ndiyo kuna utulivu na mafanikio makubwa.
Jali mambo yako ya ndani, ya nje ni usumbufu. Mambo yako ndiyo yatakupa kile unachotaka lakini ya watu yatakupotezea kile unachotaka. Kata kamba ya kufuatilia mambo ya watu na tengeneza nidhamu ya maisha yako na ishi maisha yako.
Jitoe kabisa katika mitandao inayokupa kelele, ule muda ambao ulikuwa uko bize kufuatilia mambo ya watu hebu uelekeze katika mambo muhimu yatakayokusaidia kukutoa hapo ulipo na kwenda kule unakotaka kwenda.
Hutoweza kufanikiwa kama umekuwa ni mtu wa kufuatilia mambo ya watu kila siku. Kila habari ni wewe unataka uijue. Unakuwa na hofu ya kutotaka kupitwa na habari yoyote. Kuwa na hofu ya kutopitwa na mambo yako binafsi na siyo yale ambayo hayana mchango kwako.
SOMA; Mwaka 2019 Punguza Kula Na Ongeza Kuzalisha Ili Kupiga Hatua Zaidi.
Hatua ya kuchukua leo, jifuatilie mwenyewe kabla hujaanza kufuatilia maisha ya watu. Kabla hujaanza kufuatilia mambo ya watu kaa chini na fanya kazi ambazo unapaswa kufanya.
Kwahiyo, maisha ya kujikimbia siyo mazuri, yaani yale ya kukimbia majukumu yako na kuanza kufuatilia ya wengine. Maisha ni mafupi sana kama kila mtu akianza kufuatilia maisha ya mwenzake. Jali yako na mafanikio unayoyataka yatakuja tu yenyewe.
Makala hii imeandikwa na
Deogratius Kessy, ambaye ni mwandishi, mwalimu na mjasiriamali. Unaweza pia kujifunza mengi kutoka kwake kupitia mafundisho anayoendelea kuyatoa kupitia mtandao wake wa www.mtaalamu.net/kessydeo
Ukawe na siku bora sana rafiki.
Rafiki na mwalimu wako,
Mwl, Deogratius kessy
0717101505/0767101504
deokessy.dk@gmail.com // kessydeo@mtaalamu.net
Asante sana