“A podium and a prison is each a place, one high and the other low, but in either place your freedom of choice can be maintained if you so wish.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.6.25

Ni siku nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu rafiki,
Tumeipata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari POPOTE UNAPOKUWA, MAAMUZI NI YAKO…
Maisha yanaweza kutuweka kwenye sehemu tofauti tofauti,
Yanaweza kutuweka juu sana na wakati mwingine yakatuweka chini mno.
Yanaweza kutuweka kwenye kiti cha heshima na wakati mwingine yakatuweka gerezani.
Yanaweza kutuweka kwenye utajiri mkubwa na wakati mwingine yakatuweka kwenye umasikini wa hali ya juu.

Karika hali zote hizi, kuna kitu kimoja ambacho kinabaki ndani yako, ambacho hakiwezi kuathiriwa na chochote kinachoendelea kwenye maisha yako.
Kitu hicho ni UHURU WAKO WA KUCHAGUA UFIKIRI NINI.
Unaweza kunyimwa kila kitu, ukafungwa kila kitu lakini hakuna awezaye kukufunga au kukuzuia usifikiri kile unachotaka kufikiri.
Na huu ndiyo uhuru wa kweli kwenye maisha, huu ndiyo uhuru unaoweza kututoa popote tulipo sasa na kutufikisha tunakotaka kufika.

Usikubali mazingira yoyote unayopitia sasa au utakayokutana nayo siku za mbeleni yaathiri uhuru wako wa kufikiri.
Mara zote dhibiti fikra zako, fikiria kile unachotaka na aina ya maisha unayotaka, bila ya kujali kwa sasa una maisha ya aina gani.

Falsafa ya ustoa inatukumbusha kile kilicho ndani ya uwezo wetu, ambacho ni fikra zetu. Tukitumie vizuri kwa kuwa ndiyo kitu pekee kitakachotuweka huru kwenye maisha yetu.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia uhuru wako wa fikra kufikiri chochote unachotaka bila ya kujali uko wapi kwa sasa au unapitia nini.
#UhuruWaFikra, #FikiriUnachotaka, #HaliUliyonayoInapita

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha