“Let’s pass over to the really rich—how often the occasions they look just like the poor! When they travel abroad they must restrict their baggage, and when haste is necessary, they dismiss their entourage. And those who are in the army, how few of their possessions they get to keep . . .”
—SENECA, ON CONSOLATION TO HELVIA, 12. 1.b–2

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UKWELI KUHUSU FEDHA…
Mara nyingi huwa tunafikiri kwamba tukishakuwa na fedha nyingi basi tutaweza kutatua matatizo yote tuliyonayo.
Au tukiwa na fedha nyingi basi hatutakutana na changamoto ambazo tunakutana nazo kila siku.
Utafikiri hivyo mpaka pale unapopata fedha nyingi na kugundua hakuna mabadiliko makubwa sana ndani yako.

Pamoja na kuwa na fedha nyingi unagundua kwamba kuna matatizo huwezi kuyatatua.
Pamojw na kuwa na fedha zaidi ya unavyohitaji unagundua wingi huo wa fedha unakuja na changamoto zake.
Hapa ndipo unapopata funzo kubwa kuhusu maisha na fedha, kwamba fedha ni kichocheo tu cha kile ambacho tayari kipo ndani ya mtu.
Kadiri unavyokuwa na fedha zaidi, ndivyo kile kilichopo ndani yako kinavyokuwa zaidi.

Fedha ni muhimu mno kwenye maisha yetu, lakini lazima tujue mipaka yake iko wapi, tujue ukomo wa nguvu yake na tujue wapi panahitaji nguvu zetu binafsi, hasa ule uwezo mkubwa uliopo ndani ya kila mmoja wetu.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia fedha kwa mambo yanayohusu fedha na kutumia uwezo wako wa ndani kwa mambo yanayohitaji uwezo huo.
#FedhaNiKichocheo, #TumiaUwezoWaNdani, #JuaMipakaYaFedha

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha