“Keep this thought handy when you feel a fit of rage coming on—it isn’t manly to be enraged. Rather, gentleness and civility are more human, and therefore manlier. A real man doesn’t give way to anger and discontent, and such a person has strength, courage, and endurance—unlike the angry and complaining. The nearer a man comes to a calm mind, the closer he is to strength.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 11.18.5b
Hongera sana rafiki yangu kwa nafasi hii nyingine nzuri ambayo tumeipata leo.
Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NGUVU ZAKO ZIPO KWENYE UTULIVU WAKO…
Kumbuka hili kila unapoanza kupata hisia kali za hasira, kwamba siyo utu kuwa ma hasira. Bali upole na kujali ni utu zaidi.
Mtu kamili hakubali kutawaliwa na hasira au kutoridhika badala yake anakuwa na utulivu, ujasiri, nguvu na uvumilivu.
Kadiri unavyokaribia utulivu ndivyo unavyoweza kuzifikia nguvu zako zaidi.
Kitu kimoja ambacho kimekuwa kinawaangusha wengi ni kushindwa kudhibiti hisia zao, hasa hisia kali za hasira.
Wengi wamekuwa wanajikuta wanafanya mambo ya hivyo kwa sababu ya hisia za hasira, wanasema maneno ambayo baadaye wanayajutia na kufanya vitu ambavyo baadaye wanatamani wasingefanya.
Pia kwa watu kujua jinsi hasira zinavyoweza kuwasukuma watu kufanya mambo ambayo watayajutia, wamekuwa wanachochea hisia za hasira kwa wengine.
Yaani kuna watu wanakuwekew mitego ili upate hasirs na ufanye maamuzi ya hivyo ambayo yatawanufaisha wao zaidi.
Mara zote kazana kudhibiti hisia zako, kuwa na utulivu hata kama umekutana na hali ya kukasirisha kiasi gani. Kwa sababu hatua yoyote itakayochukua ukiwa na hasira, utakuja kuijutia.
Kuwa na utulivu mara zote na hapo utakuwa na nguvu kubwa ndani yako. Hata wanaokutega uingie kwenye hasira siyo tu watashindwa, bali watakuogopa kabisa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutuliza na kutawala hisia zako na kutoruhusu hasira ikutawale au ikusukume kufanya maamuzi yoyote.
#HasiraHasara, #NguvuIpoKwenyeUtulivu, #UnapokuwaNaHasiraTulia
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha