“You cry, I’m suffering severe pain! Are you then relieved from feeling it, if you bear it in an unmanly way?”
—SENECA, MORAL LETTERS, 78.17

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari JE HAYO UNAYOFANYA YANAONDOA MAUMIVU?
Mtu unapokuwa na maumivu, kuna mambo mengi ambayo unasukumwa kuyafanya.
Unaweza kulia, kupiga kelele, kuwajibu wengine vibaya, kiharibu vitu na kadhalika.
Haya yote mtu unayafanya kwa hisia kali ambazo unakuwa nazo.
Lakini je kwa kufanya jambo hayo, kunapunguza maumivu ambayo mtu unayo?

Hili ni swali muhimu la kujiuliza kabla hujaendelea kuchukua hatua hizo ambazo zinakuzidishia maumivu zaidi kuliko kuyaondoa.
Kwa kuwa unachukua hatua hizo kwa kusukumwa na hisia, unazidi kuharibu zaidi na kujisababishia maumivu zaidi.

Kulalamika kwamba una maumivu, kutaka kila mtu ajue maumivu uliyonayo na kufanya mengine ya kusukumwa na hisia hakusaidii chochote kwenye mwumivu unayokuwa nayo.
Kinachosaidia ni kukabili kile kinacholeta maumivu na kuweka sawa kile ambacho hakijakaa vizuri.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukabiliana na maumivu unayokutana nayo kwa njia sahihi, badala ya kusukumwa na hisia.
#YakabiliMaumivu, #UsiweMtumwaWaHisia, #JiulizeKamaUnachofanyaKinasaidia

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha