“Our soul is sometimes a king, and sometimes a tyrant. A king, by attending to what is honorable, protects the good health of the body in its care, and gives it no base or sordid command. But an uncontrolled, desire-fueled, over-indulged soul is turned from a king into that most feared and detested thing—a tyrant.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 114.24
Tumepata nafasi nyingine nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Ni fursa bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MFALME AU DIKTETA?
Nafsi zetu kuna wakati zinakuwa mfalme kwetu na kuna wakati zinakuwa dikteta kwetu.
Zinakuwa mfalme pale ambapo tunafanya mambo mazuri na yenye maana kwetu, mambo yanayolinda afya za miili yetu na kutokuuendesha mwili kwa amri za kufanya yasiyo muhimu.
Nafsi zetu zinakuwa dikteta kwetu pale ambapo zinakuwa hazijadhibitiwa, zinapokuwa zinaongozwa na tamaa na kutaka kupata yale yasiyo muhimu. Hapa nafsi inakuwa dikteta asiyeshikika, kwa sababu inajali yale inayotaka pekee, iwe ni mazuri au siyo mazuri, muhimu au siyo muhimu.
Dhibiti nafsi yako ili iwe mfalme kwako na siyo dikteta kwako. Nafsi zetu zina nguvu kubwa sana ambapo tukiweza kuzidhibiti na kuziongoza vizuri, tutaweza kupiga hatua kubwa.
Lakini tunaposhindwa kuzidhibiti, basi nguvu hiyo kubwa inageuka kuwa uharibifu kwetu.
Ni kama ulivyo moto, udhibiti vizuri na utakufanyia vitu vingi na vizuri, lakini shindwa kuudhibiti na utaunguza kila kitu bila ya kujali umuhimu wake.
Ukawenna siku bora sana ya leo, siku ya kuidhibiti nafsi yako ili iweze kuhangaika na yale muhimu kwako kuweza kuwa na maisha bora. Kuwa mfalme wa nafsi na maisha yako.
#DhibitiFikraZako, #TunzaNguvuZakoKwaYaliyoMuhimu, #HangaikaNaYaliyoMuhimu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha