“Keep constant guard over your perceptions, for it is no small thing you are protecting, but your respect, trustworthiness and steadiness, peace of mind, freedom from pain and fear, in a word your freedom. For what would you sell these things?”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.3.6b–8
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni fursa bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari LINDA AMANI YA AKILI YAKO.
Weka ulinzi mkali kwenye mtazamo wako, kwa sababu hicho ndiyo kitu muhimu sana kwako kulinda.
Ni heshima yako, uaminifu wako na utulivu, ni utulivu wa akili yako, uhuru dhidi ya hofu na maumivu.
Amani ya akili yako ndiyo uhuru wa maisha yako, kitu pekee chenye thamani kubwa sana kwenye maisha yako.
Yapo mambo mengi ambayo tumekuwa tunaruhusu yatusumbue kwenye maisha yetu, ambayo tumeyapa muda na umakini wetu, lakini hayana mchango wowote zaidi ya kuvuruga utulivu na amani iloyopo ndani yetu.
Sasa tunapaswa kuwa walinzi wakubwa wa utulivu na amani ya akili na nafsi zetu.
Kutokukubali wala kuruhusu vitu vidogo vidogo vitusumbue na kutuvuruga.
Pale kitu kidogo kinapojaribu kuvuruga utulivu wako, jiulize je ndiyo kitu muhimu zaidi?
Je kama unachohofia kitatokea kimetokea kweli, utakuwa ndiyo mwisho wa maisha?
Kwa mengi tunayohofia huwa hata hayatokei, na pale yanapotokea huwa siyo makubwa kama tulivyoyajenga kwenye hofu zetu.
Hivyo kabla ya kuruhusu kitu kisumbue utulivu wako, hakikisha ni muhimu kweli.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kulinda sana utulivu na amani ya akili na nafasi yako.
#LindaAmaniYako, #HofuNiMaumivuYaKujitakia, #HangaikaNaYaleMuhimuKwako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha