Rafiki yangu mpendwa,

Ninayo furaha kukufahamisha ya kwamba, baada ya kutafakari kwa kina ili kupata njia bora kabisa ya kukushirikisha maarifa mengi ninayoyapata kwenye usomaji wa vitabu, nimepata wazo la kuwa na channel maalumu kwenye mtandao wa TELEGRAM ambayo inaitwa TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA.

Hii ni channel maalumu ya kitabu cha TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA pamoja na makala za tano za juma, ambazo kwa sasa ninachambua kwa kina kitabu kimoja kwenye kila juma.

Kupitia channel hii utaweza kupata vitabu 52 vya kusoma kwa majuma 52 ya mwaka, pamoja na kupata mafunzo ya ziada (MAKINIKIA) kutoka kwenye kitabu kilichochambuliwa.

soma zaidi kuona zaidi

Kwa kuwa ndani ya channel hii, kila juma utapata nyaraka tatu muhimu;

MOJA; Makala ya tano za juma ambayo imefanyiwa uchambuzi wa kina wa kitabu nilichosoma kwenye juma husika.

MBILI; Mafunzo ya ziada kutoka kwenye kitabu nilichosoma. Ninaposoma kitabu na kuchambua, siyo mambo yote yanapata nafasi ya kuingia. Hivyo kuna mengine mazuri yanakuwa hayajapata nafasi, haya nakupa kama mafunzo ya ziada na tutakuwa tunayaita MAKINIKIA YA KITABU CHA JUMA.

TATU; Kitabu ambacho nimesoma na kuchambua kwenye juma husika. Hapa utapata kitabu hicho na kuweza kujisomea mwenyewe kama utahitaji kufanya hivyo.

Nyaraka zote hizi tatu utazipata kwa mfumo wa nakala tete (pdf) na utaweza kuzitunza na hata kuzichapa kwa matumizi yako ya baadaye.

JINSI YA KUSHIRIKI KWENYE CHANNEL HII.

Kujiunga na channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA ni bure kabisa kwa wiki moja, ambapo utapata mafunzo hayo muhimu.

Baada ya wiki ya kwanza kuisha, kama utapenda kuendelea kuwa kwenye channel ya TANO ZA MAJUMA YA MWAKA utapaswa kulipia shilingi elfu moja (1,000/=) kila juma.

Hii ni ada ndogo ambayo itakuwezesha kuendelea kupata uchambuzi wa vitabu kila juma, kupata kitabu kilichochambuliwa kila juma na pia kupata mafunzo ya ziada (MAKINIKIA) yanayopatikana kwenye kitabu cha juma kilichochambuliwa.

Ada ya kuwa kwenye channel hii unaweza kuchagua kulipa kila wiki, au ukalipa kwa mwezi, miezi mitatu, sita au mwaka mzima. Na kadiri unavyochagua kulipa ada ya muda mrefu ndivyo ada inavyozidi kupungua na kuwa nafuu zaidi kwako.

Kama unalipa kwa wiki basi siku ya kulipa ni siku ya kwanza ya wiki ambayo ni jumatatu. Kila jumatatu utalipia tsh elfu moja (1,000/=) ili kuendelea kupata mafunzo kwenye channel hii.

Kama utalipa kwa mwezi basi utalipa siku ya kwanza ya mwezi ambayo ni tarehe moja ya mwezi husika. Kila tarehe moja ya mwezi utalipia tsh elfu tatu (3,000/=) ambayo itakupa nafasi ya kujifunza kwa mwezi mzima. Ukilipa kwa mwezi unaokoa shilingi elfu moja mpaka elfu mbili.

Na kama utachagua kulipa kwa mwaka mzima ili usisumbuke kutuma kidogo kidogo kila wiki au kila mwezi, itakuwa bora zaidi kwako. Kila mwanzo wa mwaka utalipa tsh elfu thelathini (30,000/=) ambayo itakupa nafasi ya kujifunza kwa mwaka mzima. Ukilipa ada ya mwaka unaokoa tsh 22,000/= ukilinganisha na kulipa kila wiki.

NAMBA ZA KUFANYA MALIPO.

Kujiunga na channel hii ni bure kwa wiki ya kwanza, hivyo tuma ujumbe kwa njia ya telegram kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba unapenda kujiunga na TANO ZA JUMA.

Baada ya wiki ya kwanza kuisha, utachagua kama utapenda kubaki na kuendelea kupata mafunzo haya ya uchambuzi wa vitabu na tano za juma. Kama utachagua kubaki na kupata mafunzo, utachagua unalipia kwa kipindi gani na hapo unafanya malipo na kuendelea kuwa ndani ya channel.

Malipo ya kujiunga na kupata mafunzo ya channel ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA, yafanyike kwa namba zifuatazo;

MPESA; 0755 953 887.

TIGO PESA/AIRTEL MONEY; 0717 396 253.

Ukishatuma malipo, tuma ujumbe kwa telegram kwenda namba 0717396253 ukiwa na majina yako na kwamba umelipia TANO ZA JUMA.

Karibu sana kwenye channel hii ya TANO ZA MAJUMA 52 YA MWAKA, hii ni channel yako ya kupata uchambuzi wa kina wa vitabu, kuondoka na hatua za kuchukua ili maisha yako yawe bora zaidi.

Kujiunga na channel ya TANO ZA MAJUKA 52 YA MWAKA, tuma ujumbe kwa kutumia TELEGRAM kwenda namba 0717396253 na utaunganishwa bure kwa wiki moja na baada ya hapo utachagua kama utalipia kwa wiki, mwezi au mwaka.

Karibu sana tujifunze kwa pamoja kupitia usomaji na uchambuzi wa vitabu.

Wako rafiki katika safari ya kufikia mafanikio makubwa,

Kocha Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha