“This is the true athlete—the person in rigorous training against false impressions. Remain firm, you who suffer, don’t be kidnapped by your impressions! The struggle is great, the task divine—to gain mastery, freedom, happiness, and tranquility.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.18.27–28
Ni bahati iliyoje kwetu kuweza kuiona siku hii nzuri sana ya leo,
Hayujaiona kwa sababu tu wajanja sana, kwa kuwa wapo wengi ambao hawajaiona. Au wameiona wakiwa kwenye hali isiyowawezesha kuitumia siku hii vyema.
Hivyo njia pekee ya kushukuru kwa nafasi hii ya kipekee tuliyopata, ni kuitumia nafasi hii vizuri, kufanya yaliyo sahihi na muhimu na kutokupoteza hata dakika moja.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIANDAE KWA DHORUBA…
Mwanariadha makini hasubiri mpaka siku ya mashindano ndiyo ajiandae, badala yake anatumia kila siku kwa maandalizi, hata kama mashindano yako mbali.
Kwa kuwa anajua kama hatajiandaa kila siku, basi atakuwa dhaifu na mashindano yakijitokeza atapoteza kabisa.
Hivi ndivyo tunavyopaswa kuyaishi maisha yetu kila siku, kujiandaa kwa dhoruba kabla haijatufika.
Tunawaona wengine wanaingia kwenye matatizo makubwa, kuna wakati tunafikiri sisi tuna kinga ya kutoingia kwenye matatizo hayo, tunajidanganya.
Chochote kinachoweza kutokea kwa wengine, kinaweza kutokea kwetu pia.
Hivyo kila siku unahitaji kuwa na maandalizi bora kwa dhoruba yoyote unayoweza kukutana nayo.
Usikubali mambo kuwa mazuri kukugeuze wewe kuwa dhaifu, wengi hujisahau sana pale mambo yanapokwenda vizuri, kwako isiwe hivyo.
Na pale mambo yanapokwenda tofauti na ulivyopanga, usishtuke kama vile ni kitu ambacho hakiwezekani.
Pata muda wa kutafakari maisha bila ya vile ulivyozoea, tafakari maisha bila ya wale uliowazoea, kwa sababu ipo siku vitu na watu uliowazoea hawatakuwepo.
Pia mara kwa mara jinyime vitu ambavyo vipo ndani ya uwezo wako kupata na hilo litakuimarisha hata pale ambapo vitakuwa nje ya uwezo wako kupata.
Hujui dhoruba itakufikia lini, lakini kwa hakika itakufikia. Unachohitaji sasa ni maandalizi bora ili inapokifikia isiwe kikwazo kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya maandalizi dhidi ya dhoruba yoyote unayoweza kukutana nayo.
#MipangoSiMatumizi, #JiandaeKwaUsiyotegemea, #KuwaImaraMaraZote
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha