“The soul is like a bowl of water, and our impressions are like the ray of light falling upon the water. When the water is troubled, it appears that the light itself is moved too, but it isn’t. So, when a person loses their composure it isn’t their skills and virtues that are troubled, but the spirit in which they exist, and when that spirit calms down so do those things.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.3.20–22

Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Ni fursa ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari UNAPOPOTEZA UDHIBITI WAKO…
Pale inapotokea ikawa umepoteza udhibiti wako, labda umepatwa na tamaa au umepatwa na hasira, haimaanishi kwamba wewe umepotea au nafsi yako imepotea. Bali umepoteza udhibiti wako kwa muda.
Na jawabu ni kurejesha udhibiti wako, kwenye fikra zako ha hisia zako.

Yapo mambo mengi yanayoweza kukuvuruga kwenye maisha yako, lakini kinachoanza kuvurugika ni hisia na fikra zako kabla ya maisha yako kuvurugika.
Hivyo kuwa askari mzuri wa fikra zako na hisia zako, pale unapotetereka na kujikuta umeanguka, basi simama tena kwa kurudisha udhibiti wako.

Kama mwanga wa jua unamulika dunia, halafu wingu likapita na kuzuia mwaka huo usimulike, haimaanishi kwamba jua limezima, ila tu wingu limepita.
Na hakuna wingu ambalo limewahi kuziba jua milele, kila wingu linapita, ni la muda tu.

Chukulia hivi kwenye nyakati ambazo unapoteza udhibiti wako, ona nyakati hizo kama wingu kwenye mwanga wa jua. Wewe kama jua unabaki imara, lakini fikra na hisia zako zinakuwa zimevurugwa kwa muda. Ni wajibu wako kurudisha udhibiti ili maisha yako yaweze kwenda vyema.

Ukawe na siku bora sana ya leom siku ya kurejesha udhibiti wako pale unapoupoteza na kutokutana tamaa na kujiona hufai.
#DhibitiHisiaZako, #TawalaFikraZako, #RejeshaUtulivuUnapopotea

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha