“Above all, it is necessary for a person to have a true self-estimate, for we commonly think we can do more than we really can.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 5.2

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni siku mpya na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari JITATHMINI KWA USAHIHI…
Moja ya makosa ambayo wengi tunafanya ni kushindwa kujitathmini kwa usahihi, au kutokujitathmini kabisa.
Tunaenda maisha yetu yote bila ya kuwa na uelewa sahihi wa nini tunaweza na wapi madhaifu yetu yalipo.

Kwa kushindwa kujitathmini, tunaanguka kwenye makosa makubwa mawili,
Moja; tunajikweza kwenye baadhi ya maeneo, tunaona tunaweza sana kumbe siyo.
Mbili; tunajishusha kwenye baadhi ya maeneo, kwa kuona hatuwezi kumbe tuna uwezo mkubwa.

Wengi wamekuwa hawapendi kujitathmini kwa sababu wanahofia kugundua vitu ambavyo vitawakatisha tamaa, hivyo wanaona njia pekee ni kutokujitathmini kabisa.

Chukua muda wa kujitathmini kwa kina na kwa usahihi leo, ujue maeneo yapi una uimara na uko vizuri. Pia ujue maeneo yapi una udhaifu.
Ukishajua hili, peleka nguvu zako zote kwenye maeneo ambayo una uimara, na kwa yale ambayo una idhaifu, tafuta mtu mwenye uimara ushirikiane naye.
Maana kosa jingine kubwa ni kutaka kujiimarisha kwenye udhaifu, kitu kitakachopelekea uwe na udhaifu imara zaidi.

Jitathmini kwenye maisha yako, kazi yako, biashara yako na kila unachofanya. Kujijua wewe mwenyewe kwanza ni hatua muhimu kwa mafanikio yako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujitathmini kwa usahihi na kuchukua hatua sahihi ili kuyaboresha maisha yako.
#JitathminiKwaUsahihi, #PimaMaishaYako, #JijueMwenyeweKwanza

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha