“We can remove most sins if we have a witness standing by as we are about to go wrong. The soul should have someone it can respect, by whose example it can make its inner sanctum more inviolable. Happy is the person who can improve others, not only when present, but even when in their thoughts!”
—SENECA, MORAL LETTERS, 11.9

Amka mwanamafanikio,
Amka kwenye siku hii mpya, bora na ya kipekee sana kwetu.
Amka na uiendee siku hii kwa hamasa kubwa, uende ukachukue hatua kubwa sana ili uweze kupata matokeo bora sana.

Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari; CHAGUA MTU WA KUJIPIMA NAYE…
Kinachofanya tuamini kwamba sisi binadamu ni wanafiki ni pale tunapokuwa mbele ya wengine tunafanya yaliyo sahihi, lakini tunapokuwa wenyewe tunafanya yasiyo sahihi, tukijua hakuna anayeona.
Hivyo licha ya kuonekana tunafanya yaliyo sahihi, tunashindwa kupiga hatua kwa sababu tunakosa msimamo.

Ili kuondokana na hali hii, unapaswa kichagua mtu ambaye uyajipima naye, huyu ni mtu unayemheshimu, ambaye unapenda sana misimamo yake na kujipima wewe kama unaweza kuishi kama yeye.
Mtu huyo anaweza kuwa hai au alishakufa, anaweza kuwa mtu halisi au wa kutengeneza.

Muhimu ni uwe na kitu cha kukupima kwenye kila unachofanya.
Kwa kila hatua unayochukua, iwe mbele ya wengine au ukiwa mwenyewe, chukulia kwamba mtu yule unayejipama naye anaiona. Na hapo jiulize je atachukuliaje wewe kufanya hicho ulichofanya.
Kwa kuwa na mtu wa kujipima naye kama hivi, ni rahisi kwako kufanya yake yaliyo sahihi mara zote, iwe uko mbele ya wengine au uko peke yako.

Chagua leo nani utakayejipima naye, ili kukazana kuyaboresha maisha yako zaidi kila siku.
Na kama utayaishi maisha yako vizuri, huenda wengine wakakuchagua wewe kama mtu wa kujipima na maisha yao.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutafakari kabla hujafanya chochote, kwa kujipima na yule unayemheshimu sana.
#JipimeNaWakuuKufikiaUkuu, #UsijidanganyeMwenyewe, #FanyaKilaKituKamaUnaonekanaNaKilaMtu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha