“The unrestricted person, who has in hand what they will in all events, is free. But anyone who can be restricted, coerced, or pushed into something against what they will is a slave.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 4.1.128b–129a

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana leo.
Tumepata nafasi ya kipekee leo kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari; ISHI BILA KIZUIZI…
Mtu asiye na kizuizi, ambaye ana kila anachotaka katika hali yoyote ndiye mtu aliye huru.
Yeyote ambaye anaweza kuzuiwa, kulazimishwa au kusukumwa kinyume na matakwa yake ni mtumwa.
Uhuru kwenye maisha ni wewe kuwa mwamuzi mkuu wa maisha yako, kuweza kufanya maamuzi ya kipi muhimu zaidi kwako na kipi siyo muhimu.
Upo huru pale unapoweza kuchagua ufanye au usifanye nini kulingana na matakwa yako, na siyo kulazimika kufanya au kutokufanya kitu kwa sababu kila mtu anafanya.

Tumekuwa tunapoteza uhuru wetu bila ya sisi wenyewe kujua, hasa pale tunapokuwa tunategemea watu wengine wafanye vitu kwa ajili yetu.
Na hata kwa wengi, mpango wa kufikia mafanikio makubwa umewageuza kuwa watumwa wa kile wanachofanya au watumwa wa wengine.

Maisha bora ni yale ambayo mtu upo huru, yale ambayo unachagua kufanya na siyo inakubidi ufanye.
Unaweza kuwa na maisha haya kama utachagua kuishi kwa misingi sahihi na siyo kwa kuwafurahisha wengine.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na maisha yasiyo na kizuizi, siku ya kuwa huru na maisha yako.
#IshiBilaKizuizi, #ChaguaKuwaHuru, #UsijiwekeKwenyeGereza

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha