“Zeno would also say that nothing is more hostile to a firm grasp on knowledge than self-deception.”
—DIOGENES LAERTIUS, LIVES OF THE EMINENT PHILOSOPHERS, 7.23

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari ADUI YAKO MKUBWA NI KUJIDANGANYA MWENYEWE…
Adui mkubwa kabisa kwenye maisha yako, ni kujidanganya wewe mwenyewe.
Huyu ni adui ambaye amekuwa kikwazo kwako kuweza kupiga hatua na kupata unachotaka.
Adui yako mkubwa kwenye kujifunza zaidi ni kuamini kwamba tayari unajua kila kitu, hapo unakosa kujifunza mazuri zaidi.
Adui yako mkubwa kwenye kupata zaidi ya ulivyonavyo sasa ni kuamini kwamba umeshapata kila kitu.

Mafanikio kwenye maisha yanakuja pale tunapokuwa wa kweli kwetu wenyewe.
Pale tunapokubali kwamba hatujui na hivyo tukajifunza.
Pale tunapokubali kuna vitu hatuna na hivyo kupata zaidi.

Haijalishi unajua kiasi gani, kuna vitu vingi mno unavyoweza kujifunza.
Haijalishi umepiga hatua kiasi gani, unaweza kupiga hatua zaidi ya hapo ulipo sasa.
Acha kujidanganya na ukabili unalisia kama ulivyo, utaweza kupiga hatua zaidi kupitia uhalisia kuliko kupitia kujidanganya.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuacha kujidanganya na kuukabili ukweli kama ulivyo, hata kama unakuumiza.
#AchaKujidanganya, #UnaMengiYaKujifunza, #UnaHatuaZaidiZaKupiga

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha