“Hold sacred your capacity for understanding. For in it is all, that our ruling principle won’t allow anything to enter that is either inconsistent with nature or with the constitution of a logical creature. It’s what demands due diligence, care for others, and obedience to God.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 3.9
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari SEHEMU TAKATIFU KWAKO…
Akili yako ndiyo sehemu takatifu sana kwako,
Ni akili yako ndiyo inayokutofautisha wewe na wanyama wengine.
Uwezo wako wa kufikiri ndiyo unakufanya wewe kuwa mwanadamu.
Hivyo akili yako na uwezo wako wa kufikiri ni sehemu takatifu sana kwako, ambayo hupaswi kuruhusu uchafu wowote uingie.
Usiruhusu taarifa hasi kuingia kwenye akili yako,
Usiruhusu fikra za chuki, wivu na vinyongo kutawala akili yako.
Usiruhusu mambo yasiyo na manufaa kwako kutawala akili yako.
Hii ni sehemu takatifu kwako, ambayo unapaswa kuilinda kwa umakini mkubwa na kuitumia kwa yale muhimu zaidi kwako.
Tumia akili yako kufikiri yale muhimu kwako, yale yanayokufanya uwe bora zaidi, yale yanayokuwezesha kupiga hatua zaidi na yale yanayokuwa na msaada kwa wengine.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kulinda eneo takatifu kwako kwa kuruhusu yale masafi pekee kutawala fikra zako.
#DhibitiFikraZako, #FikiriChanya, #AkiliNiEneoTakatifuKwako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha