“You are not your body and hair-style, but your capacity for choosing well. If your choices are beautiful, so too will you be.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.1.39b–40a
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UZURI WA KUCHAGUA…
Wewe siyo mwili wako, na wala siyo mali ulizonazo, wala chochote unachojitambulisha nacho.
Wewe ni matokeo ya kile unachochagua kwenye maisha yako.
Unayajenga au kuyabomoa maisha yako kwa machaguo unayofanya kila siku ya maisha yako.
Hivyo unochagua vizuri unakuwa na maisha mazuri.
Lakini unapochagua vibaya, unakuwa na maisha mabaya.
Uchaguzi wako ni matokeo ya uwezo wako wa kufikiri pia,
Hivyo unapofikiri vizuri unachagua vizuri.
Kazana kujijengea maisha bora kwa kufikiri vizuri na kuchagua vizuri.
Unaweza kuchagua kuwa huru kwa fikra zako na machaguo yako, au ukachagua kufikiri na kufanya kile ambacho kila mtu anafanya.
Lakini unapaswa kujua, ni wewe pekee uliyejifikisha hapo ulipo sasa, kwa fikra na machaguo uliyofanya huko nyuma.
Na fikra na machaguo unayofanya leo, ndiyo yanayoitengeneza kesho yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufikiri vyema, ili kuchagua vizuri na uwe na maisha bora.
#MaishaNiKuchagua, #UnapataUnachotafuta, #WeweNdiyeNahodhaWaMaishaYako
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha