“I may wish to be free from torture, but if the time comes for me to endure it, I’ll wish to bear it courageously with bravery and honor. Wouldn’t I prefer not to fall into war? But if war does befall me, I’ll wish to carry nobly the wounds, starvation, and other necessities of war. Neither am I so crazy as to desire illness, but if I must suffer illness, I’ll wish to do nothing rash or dishonorable. The point is not to wish for these adversities, but for the virtue that makes adversities bearable.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 67.4
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KUWA TAYARI WAKATI WOWOTE…
Hakuna mtu ambaye anapenda magumu yatokee kwenye maisha yake,
Hakuna anayependa kukumbwa na maradhi,
Hakuna anayependa kushindwa kwenye chochote anachofanya,
Lakini vitu hivi vinatokea kila mara na vinatokea kwa wengi.
Hii ni kusema kwamba licha ya kutokupenda vitu hivi, kuna wakati votatokea kwako pia, kwa sababu havitokei kwa mipango ya mtu, bali vinatokea kama vinavyotokea.
Hivyo licha ya kuchukua kila aina ya tahadhari ili mambo hayo tusiyoyataka yatokee, bado hatuwezi kuyaepuka kwa asilimia 100.
Unaweza kujiandaa vizuri kwa kila unachofanya kuepuka ugumu, lakini kikatokea kitu ambacho hukitegemea.
Unaweza kulinda afya yako vizuri, ukala kwa afya na kufanya mazoezi kila siku, lakini ukakumbwa na ugonjwa usiotarajia.
Na unaweza kujitoa kupita uwezo wako, ukajitahidi sana ili usishindwe popote na bado kikatokea kitu kinachofanya ushindwe.
Jawabu la yote haya ni kuwa tayari wakati wowote, kuwa tayari kupokea hali ambayo hukuitegemea, ambayo uliifanyia kazi ili kuikwepa lakini ikatokea bila ya matarajio yako.
Kuwa tayari kupokea hali za namna hii na kuzitumia kama njia ya wewe kupiga hatua zaidi.
Mambo kama haya yanapokukuta umejiandaa kuyapokea hayakutetereshi na yanazidi kukufanya kuwa imara.
Lakini manbo haya yanapokukuta kwa mshangao, ukiwa huna maandalizi, yatakuangusha kabisa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa tayari kwa chochote wakati wowote.
#JiandaeKwaUsiyotegemea, #MipangoSiMatumizi, #UsiyoyatakaYatatokea
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha