“What is it then to be properly educated? It is learning to apply our natural preconceptions to the right things according to Nature, and beyond that to separate the things that lie within our power from those that don’t.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.22.9–10a

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari DALILI ZA KUWA UMEELIMIKA KWELI…
Watu wengi hawawezi kutofautisha kusoma na kuelimika.
Wengo hufikiri kwa kuwa na cheti cha kuhitimu masomo basi wameshaelimika,
Au wakisoma vitabu vingi basi wameshaelimika.
Kuna kusoma na kuelimika, vitu viwili tofauti kabisa.

Kusoma ni kuyapata maarifa na kuyajua,
Kuelimika ni kuweza kuyatumia maarifa hayo katika kuyaganya maisha yako yawe bora zaidi.
Hivyo kama umeyapata maarifa lakini maisha yako yamebaki vile vile, umesoma lakini hujaelimika.

Kuelimika pia ni kuweza kuweka mipaka kati ya vitu vilivyo ndani ya uwezo wako na vile vilivyo nje ya uwezo wako.
Hapa pia wengi wanakwama, wakihangaika na kila kitu bila ya kuweka mipaka ya kipi kipo ndani ya uwezo wao na kipi kipo nje ya uwezo.

Usiishie tu kusoma na kuyapata maarifa, badala yake tumia kila unachojifunza kuyafanya maisha yako, na hata ya wengine kuwa bora zaidi.
Kama unajifunza kitu na hukitumii, ni sawa na umechagua kuyapoteza maisha yako.
Elimika kwa kutumia kila unachojifunza ili maisha yako yawe bora.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia kila ambacho umewahi kujifunza ili kuyaboresha maisha yako.
#KusomaSiKuelimika, #TumiaUnachojifunza, #KipimoChaUsomiNiUboraWaMaisha

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha